MAHAKAMA KUU ARUSHA KUTOA UAMUZI HATMA YA IGP,RPC, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI(AG),DC NA OCD NGORONGORO


Na Joseph Ngilisho, ARUSHA

MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha  imepanga  kutoa uamuzi, Mei 10 Mwaka huu katika kesi  ya kulazimishwa kupokea ( Enforced disappearance)kwa mzee Oriais Oleng’iyo (85) wa kijiji cha Ololosokwan, Loliondo  Wilaya ya Ngorongoro ambaye alipotea na jajulikani alipo wakati wa zoezi la uwekaji mipaka.


Wajibu maombi kwenye shauri hilo ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Mkuu wa mkoa wa  Arusha , Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC)  wa Arusha, , Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro na  Mkuu wa polisi wilaya ya Ngorongoro.


Kesi hiyo namba 67 ilikuja mahakamani Leo kwa ajili ya kusikilizwa mbele ya Jaji Mohammed Gwae ambapo waleta maombi na wajibu maombi walipata nafasi ya kuwasilisha hoja zao mbele ya mahakama hiyo.


Upande wa waleta maombi walisema Mahakama inamamlaka ya kuamuru mzee huyo kuletwa mahakamani au kuachiwa huru aidha akiwa hai au akiwa amekufa.


Simoni Mbwambo ni wakili wa Upande wa Utetezi alisema  Madai ya Kupigwa risasi na kupotezwa kwa Mzee Oriais Oleng’iyo ni matokeo ya operesheni iliyofanyika Loliondo June  10, 2022 wakati wa uwekaji vigingi (beacons) eneo la vijiji 14 vya Loliondo lenye kilometa za mraba 1502.


Mbwambo aliomba Mahakama iamuru walalamikiwa  kumleta mahakamani Oriaisi Pasilange Ng’iyo ambaye amepelekwa kusiko julikana tangu alopokamatwa nyumbani kwake Engong’u Nairowa, Kata ya Ololosokwan, Loliondo wilaya ya Ngorongoro


Hata hivyo Mbwambo alisema wameleta maombi hayo baada ya watu wengine waliokamatwa katika operesheni ya kuweka mipaka katika eneo la pori tengefu la Pololeti lililopo Ngorongoro kuachiwa na kesi yao kufutwa lakini mzee huyo hadi kufikia sasa hajulikani alipo.


Aliendelea kusema Walipoletwa mahakamani mzee Oriaisi hakuletwa mahakamani kama wenzake japokuwa shauri hilo liliondolewa mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa Jamhuri haina nia ya kuendelea na shauri hilo.


"Baada ya washtakiwa kuachiwa huru Mzee Oriaisi hakuwa miongoni mwao hivyo tukalazimika kukimbilia mahakamani kudai mzee huyo kwa kuwa polisi ndio wanajua alipo " alisema Mbwambo.


Joseph Oleshangay ni wakili wapili wa Mleta maombi  ambaye alisema  wana amini Mteja wao yupo mikononi mwa polisi kwa kuwa ndio waliomchukua siku ya vurugu zilizotokea 


Upande wa Jamhuri walipinga maombi hayo kwa kusema kuwa hakuna mahali waleta maombi  waliposema au kutaja namba ya polisi, au namba ya gari ya polisi zaidi ya kusema "difenda" ambapo inaweza kuwa gari yoyote.


Mjibu Maombi Peter Mseti alisema   hawajawahi kumshikilia mtu huyo wala jina lake halijawahi kuonekana kwenye majina ya walioshikiliwa kuanzia juni 8 hadi 20 kati ya wale waliokuwa na kesi ya mada.


"Na hoja ya kutokutoa taarifa ya kupotea kwenye vyombo vya dola mteja wetu asingeripoti kupotea wakati alikamatwa na tunaamini yupo kwenye mikono ya polisi na polisi ndio watuhumiwa ndio maana tumeamua kukimbilia  mahakamani tukiamini haki itapatikana" alisema"Oleshangay


Aidha alishindwa kuthibitisha kuwa anayeshikiliwa isivyokihalali  yupo jela ama amekufa.

Ends..

Post a Comment

0 Comments