Na Joseph Ngilisho Arusha
MBUNGE wa zamani wa Arusha,Godbless Lema (Chadema)amemwomba rais Samia Suluhu Hassan kurejesha uhuru wa biashara ya Madini ya Tanzanite, kuuzwa kwenye masoko mbalimbali ya madini hapa nchiñi ikiwemo jijini Arusha .
Akiongea na vyombo vya habari mapema leo jijini hapa Lema ,alisema hatua ya katazo la madini hayo kuuzwa kwenye masoko mbalimbali ya madini hapa nchini, lililotolewa na waziri mkuu,Kasimu Majaliwa Jilai 7,2021 limeathiri mwenendo wa uchumi ,ajira hasa kwa jiji la kitalii la Arusha .
Alisema kuzuia biashara ya Tanzanite katika masoko ya madini jiji Arusha,ni kuwanyima uhuru wafanyabiashara wa madini na nikinyume cha sera ya biashara huria lakini pia kunadhofisha biashara ya Tanzanite.
Lema alimshauri Rais Samia kuimarisha soko la ndani la mahitaji ya madini hayo na kufikia asilimia 70 na hivyo kuiwezesha serikali kujenga uchumi bila ku
"Nimwombe sana rais Samia aondoe hii marufukuu iliyowekwa ya kuzuia Tanzanite kuuzwa nje ya Mererani, nchi hii haiko kwenye dhama za ujima katazo hilo limeathiri ajira za madalali wa madini Arusha ambao wamesajiliwa na wanalipa Kodi"alisema
Lema ambaye pia ni mwenyekiti wa chadema kanda ya Kaskazini, alisema Rais Samia amekuwa alifanya kazi kubwa kuitangaza Tanzania nje ya nchi ikiwepo kuita wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nje sasa zuio hili ni kinyume na mikakati ya Rais kukuza uchumi.
"Arusha ni kituo cha utalii Afrika mashariki,Kuondoa wafanyabiashara wakubwa wa madini hayo na kupeleka Mererani ni kosa la kimkakati la kibiashara"
"Mimi naijua biashara hii nimewahi kuwa mfanyabiashara na mchimbaji wa Tanzanite…mawazo ya kuzuia biashara ya Tanzanite nje ya Mererani ni mawazo wa ujima, Tanzanite inapaswa kuuzwa mikoa yote nchini na kuifanyia promosheni kubwa ili Watanzania walau asilimia 70 wavae vidani vya Tanzanite," .
Aliongeza kuwa kama Watanzania wakiijua vizuri Tanzanite na kununua soko la ndani litakuwa kubwa na Serikali itapata fedha na Kodi nyingi zaidi kuliko kuijificha Mererani.
Lema amesema Arusha ni kitovu cha utalii Afrika ya Mashariki na watalii wengi wanafika Arusha na kuondoka hivyo Tanzanite inapaswa kuuzwa Arusha na miji mingine.
"Ni aibu leo ulienda kwenye miji mikubwa Afrika Kusini, Dubai Kenya, India na nchi nyingine ukuta Tanzanite inauzwa lakini hapa nchini miji kikubwa hakuna Tanzanite," amesema.
Alisema kuuzwa Mererani Tanzanite hakuzuiii kutoroshwa madini hayo bali utotoshwaji unaendelea na kinachopaswa kufanyiwa ni serikali kuweka Mazingira mazuri ya biashara hiyo.
"TRA iboreshe mifumo ya kodi wachimbaji waone fahari kulipa kodi kwa kupeleka madini yao kufanyiwa tathimini lakini pia Serikali inapaswa kuwa inatoa cheti maalum cha kuthibitisha uhalali wa Tanzanite (Certificate of origin) na siyo kuzuia madini kutoka Mererani au kujenga ukuta," amesema.
Kwa muda mrefu wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite jijini Arusha wamekuwa wakiomba kurejesha Arusha biashara ya Tanzanite hasa baada ya kufunguliwa soko la.madini Arusha.
Aidha alimtaka Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka kuacha mawazo ya kijamaa na ujima , kuishauri serikali kuhamishia soko la madini hayo katika mji wa Mererani ,aliwaomba wafanyabiasharawa Tanzanite kushikamana na kupigania madini hayo yaruhusiwe kuuzwa jijini Arusha.
"Kama Sendeka alishauri Tanzanite iuzwe Mererani Pekee atakuwa na fikra za ujamaa na anapaswa akachunge ng'ombe na kulea wajukuu nyumbani"alisema Lema.
Ends...
0 Comments