KIGOGO WA MADINI YA TANZANITE AFIKISHWA MAHAKAMANI WAMO PIA WACHIMBAJI WENGINE SABA ,MAHAKAMA YATAPIKA


Na Joseph Ngilisho,SIMANJIRO 


 

Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha Joel Saitoti ambaye pia ni Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Gem & Rock Venture na wenzake saba  wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kujibu Mashtaka mawili ya shambulio na kukaidi amri ya Wizara ya Madini katika tukio lililotokea march 13 mwaka huu katika Mgodi wa Kitalu C inayomilikiwa  na Serikali Mwekezaji Mzawa Onesmo Mbise.


Wakisomewa Mashitaka na Mwendesha Mashitka wa Polisi, Mosses Hamilton Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Charles Uiso ilidaiwa kuwa katika shitaka la Kwanza linalowahusu washitakiwa wote saba ilidaiwa kuwa wote kwa pamoja waliwashambulia kwa majabali na silaha za uchimbaji wafanyakazi sita wa Kampuni Franone inayochimba Mgodi wa madini ya Tanzanite kitalu C kwa kushirikiana na serikali.
 

Mbali ya Saitoti walioshitakiwa wengine ni pamoja na Petro Exsaud(48) mkazi wa Moshono Arusha,Mosses Kelerwa(45) mkazi wa Mirerani,Daniel Siyaya(44) mkazi wa Ilboru Arusha, Mosses sirikwa (46) mkazi wa Ilboru,Dausen Mollel(58) Mkazi wa Ilboru na,Enock Nanyaro(32) mkazi wa Arusha.
 

Katika shitaka la kwanza,Mwendesha Mashitaka wa Polisi alidai kuwa shitaka hilo linawahusu washitakiwa wote kwani ilidaiwa kuwa March 13 mwaka huu waliwashambulia  kwa majabali na vifaa bya uchimbaji wafanyakazi sita wa Franone akiwemo Benson Banash,Vedastus Swea,Alvin Msuya,Swetbert Albogast,Mussa Unambe na Bonfance Mollel .

Hamilton alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa Hilo wakati wakijua wazi kuwa kufanya kosa hilo nikosa kisheria lakini washitakiwa wote walikana shitakana hilo na walikidhi vigezo vya dhamana kwani kila mshitakiwa alidhaminiwa na mdhamini mmoja na bBondi ya shilingi milioni moja na washitakiwa walikidhi vigezo vya dhamana na upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika kesi hiyo itatajwa tena aprill 14 mwaka huu katika mahakama hiyo.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi , shitaka la pili linalowahusu washitakiwa wawili akiwemo  Joel Saitoti (50) ambao ilidaiwa wameshitakiwa kwa shitaka moja la kukaidi amri ya Wizara ya Madini ya ambapo ilidaiwa kuwa walizuiwa kufanya shughuli za uchimbaji baada ya mtobozano na Kitalu C lakini walikaidi na kuendelea na kazi wakati wakijua wazi ni kosa.
 
Baada ya kusomewa shtaka hilo walikana na walipewa dhamana ya mtu mmoja mmoja na kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuweka Bondi ya shilingi milioni moja .

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika na washitakiwa wataanza kusomewa Maelezo ya Awali April 14 mwaka huu.

 
Ends....

Post a Comment

0 Comments