Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WAFANYABIASHARA wa soko kuu jijini Arusha,wamehimizwa,kulipaushuru na kodi mbalimbali kwa wakati ikiwa ni pamoja na wenye maduka kuhakikisha wanakuwa na leseni kwenye maduka yao ili kuongeza mapato ya halmashauri hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Kati,jijini Arusha,Abdulrasul Tojo,kwenye mkutano wa hadhara wa maendeleo ya kata uliofanyika katika soko hilo, ikiwemo kusoma taarifa ya mapato na matumizi na kusikiliza kero za wananchi .
Tojo aliwahimiza wafanyabiashara kwenye kata hiyo kuhakikisha wanalipa kodi na ushuru ili kuiwezesha halmashauri hiyo kutoa huduma ipasavyo kwani katika kipindi cha mwaka jana 2022/23 walitenga kukusanya kiasi cha sh,bilioni 30 ,lakini waliishia kukusanya bilioni 17 pekee.
Alisema ulipaji wa kodi na ushuru umekuwa wa kusuasua na hivyo kushindwa kufikia malengo wakati soko hilo ambalo lililojengwa miaka ya 1960 lina wafanyabiashara1900 ,lakini mapato yake ni madogo kwani kwa mwezi wanakusanya sh,
milioni 48 hadi 50 na linahitaji matengenezo makubwa ya miundo mbinu yake.
Alisema katika bajeti ya mwaka huu kata hiyo itapokea shilingi bilioni2.5 kwa ajili ya shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu ya maji taka na ,mifumo ya masoko ya Samunge na soko kuu pia ukarabati utahusisha shule tatu,za msingi ambazo ni Uhuru na Meru,pia shule moja ya sekondari Arusha
Alisema ukarabati huo utahusisha,uwekaji wa taa za barabarani,ujenzi wa barabara za kati tati ya Jiji kwa kiwango cha lami
kwenye mitaa ukarabati wa mifumo ya maji ya mvu kuxibua mifereji
Akawaomba wafanyabiashara kwenye kata hiyo kuongeza kasi ya ulipaji wa kodi ,ushuru leseni za Maduka ambao unasuasua na kuwaambia kuwa halmashauri imeanzisha taskforce kukagua kila duka kama wanazo leseni,wamelipa mapato yote kwa mjibu wa sheria kwa kuwa imebainika kuna ukwepaji
Kuhusu changamoto mbalimbali,zilizoelwzwa ba wananchi wake alisema zitatatuliwa na wananchi wenyewe na kamwe hakuna mtu kutoka nje ambae atakuja kuwatatulia kero zao hivyo akawaomba washirikiane
Akawaomba wananchi kushirikiana pamoja kukemea na kupinga mapenzi ya jinsia moja kwa kuwa huo sio utamaduni wetu na ni laana pia ni kinyume na maamrisho ya mungu na jambo hilo ni hatari sana halifai kuwepo.
Awali baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu walilalamikia kero mbalimbali ikiwemo ukubwa wa kodi za maduka waliopangisha,kutokuwepo na vyoo,pamoja na mitaro ya maji kutoa harufu kali kiasi kwamba wateja wamekuwa wakikerwa na harufu hiyo na kushindwa kununua bidhaa,jambo ambalo diwani huyo aliahudi kutatua.
Ends....
0 Comments