MAPYA YAIBUKA MGODI WA MADINI YA TANZANITE KUVAMIWA NA KUPOKONYWA MADINI WANAAPOLO WALILIA RAIS SAMIA


Na Joseph Ngilisho, Arusha 


Sakata la  vurugu zilizoibuka ndani ya Mgodi wa Tanzanite wa kampuni ya Gem and Rock Venture unaomilikiwa mfanyabiashara maarufu, Joel Saitoti ,limechukua sura mpya mara baada ya meneja wa mgodi huo,  kuibuka na kudai kuwa mkaguzi wa baruti Ezekiel Isaac akiwa na watu zaidi ya 30 walivamia mgodi wao na kuwashambulia kwa kipigo na kisha kujaribu kuwapokonya madini waliozalisha siku ya tukio, kinyume cha sheria.

Akitoa ufafanuzi wa sakata hilo,lililotokea machi 13 mwaka huu,meneja wa mgodi huo Martin Msigwa alidai kuwa siku ya tukio wakiwa wanaendelea na shughuli za uzalishaji wa madini hayo mkaguzi huyo wa baruti wakiwa ameambatana na wachimbaji, waliwavamia na kuanza kuwapiga wafanyakazi wa kampuni hiyo wakilazimisha watoe madini waliokuwa wamezalisha zaidi ya kilo nne.

Alifafanua Kuwa sakata hilo ,lililotokea machi 13 mwaka huu,wakati wanaendelea na uzalishaji wa madini hayo ambapo mkaguzi huyo wakiwa na kundi la wachimbaji wengine waliwavamia na kuanza kuwapiga wafanyakazi wa kampuni ya Gem and Rock Ventures LTD wakilazimisha watoe madini waliokuwa wamezalisha zaidi ya kilo nne.

Mkaguzi huyo wa baruti  Ezekiel Isaac alifanikiwa kuvunja geti la Mtobozano akipitia mgodi wa Franone Mining  na kuingia kitalu B inayomilikiwa na  kampuni ya  Gem and rock  bila kufuata taratibu .


"Baada ya kufika alikuta shughuli za uzalishaji zikiendelea na kutaka wapatiwe madini yaliyokuwa yamezalishwa ,akilazimisha yapitie mgodi wa Kitalu C,lakini wafanyakazi wetu waligoma kuachia madini hayo wakidai sio utaratibu wa kawaida kwakuwa mkaguzi wa baruti alikuwa mwenyewe alishirikiana na wafanyakazi wa Franone ,bila kuwepo askari yoyote wa polisi,jeshi la wananchi (JWTZ) na usalama wa taifa kama ilivyozoeleka"

Mmoja ya wafanyakazi wa mgodi huo Sifael Laizer  alidai kuwa kabla ya tukio hilo Machi 10 mwaka huu majira ya saa 10 jioni meneja wetu alipokea barua iliyotumwa kupitia mtandao wa WhatsApp kutoka kwa afisa mkaguzi wa baruti Ezekiel Isaac  ikiitaka kampuni hiyo kusimamisha uzalishaji katika Kitalu B ili kupisha uchunguzi baada ya kuwepo malalamiko ya kuwepo kwa hewa chafu inayotokana na mlipuko wa baruti.


Meneja  alisema kuwa  uongozi wa mgodi huo uliamua kujibu barua hiyo kwa njia hiyo hiyo ya whatsup na vile vile aliendelea kusema kuwa wanashangaa kuwaambiwa kuwa wako kwenye eneo kitalu C wakati kampuni yao ipo kitalu B ambayo inachimba madini  zaidi ya mita 580 kutoka mgodi wa Franone kwa hiyo sio kweli kwamba moshi wa baruti unawafikia.


"Tunashangaa kuona kampuni ya Franone wakilalamika kuhusu moshi wa baruti wakati wapo umbali mkubwa na sisi kama ni hivyo kwanini migodi mingine ya jirani kama mgodi wa Deo Minja ,Sunda na Papaking hawalalamiki"???


Naye  Wilbart Mosses mfanyakazi wa mgodi huo wa Gem and Rock Ventures amesikitishwa kuona mkuu wa usalama Mererani (DCO) kutoa amri kwa watu 0⁰aliokuwa ameongozana nao kuanza kuwashambulia kwa kipigo kikali na kupokonywa madini yetu ambayo ndio ujira wetu na kuondoka nayo.Hata hivyo wafanyakazi wa Kampuni walifanikiwa kukamata baadhi ya vifaa vilivyotumika kukatia geti la Mtobozano la kampuni ya Gem and Rock Ventures Co ltd na ambavyo vipo polisi kama ushahidi. 


Mosses alimwomba rais Samia suluhu Hasan kuingilia kati sakata hilo ili kupata haki yao ya msingi kwani wamechoka kuonewa mara kwa mara pindi wanapoanza uzalishaji wa madini.


Kamanda wa polisi Mkoani  Manyara,George Katabazi alipoulizwa kwa njia ya simu alidai kuwa alidai kuwa jeshi hilo lilifika eneo la tukio baada ya kupata taarifa kuwa kunavurugu zinaendelea katika mgodi huo kitalu B.


Alisema mara baada ya kufika eneo la tukio walifanikiwa kutuliza ghasia na kuwashikiliwa vijana 21 akiwemo mmiliki wa mgodi Saitoti .


Endd...






Post a Comment

0 Comments