Na Joseph Ngilisho, Arusha
Chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) mkoa wa Arusha kimeanza maandalizi ya kumpokea aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbress Lema anayetarajiwa kutua kwa kishindo hapa nchini machi 1,mwaka huu saa sita mchana katika uwanja wa ndege wa KIA.
Akiongea na vyombo vya habari katika kikao cha maandalizi,mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha,Elisa Mungure alisema maandalizi ya kumpokeaa shukaa wao yamekamilika na wananchi zaidi ya elfu 10 wanatarajiwa kujipanga katika barabara kuu ya Arusha Moshi kutokea uwanja wa ndege Kia .
Alisema kina mama wamejipanga kumpa heshima ya aina yake kwa kutandika kanga barabarani kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, KIA hadi Arusha na wanaume walilala ili apite juu yao migongo yao ikiwa ni heshima ya kumlaki mwana mwanakondoo aliyepotea.
Alisema Lema ambaye pia Mjumbe wa kamati kuu na mwenyekiti wa chadema kanda ya kaskazini atapewa heshima kubwa ya kitaifa na ndani ya msafara wake kuna vituo zaidi ya vinne atakuwa akisimama na kusalimia wananchi .
"Leo viongozi wa chadema tumekutana kuanza maandalizi ya kumpokea kiongozi wetu na Kwa kuzingatia uwezo na upendo mkubwa wa Lema ujio wale lazima Arusha isimame na inchi nzima itasimama "
Alisema Lema ataingia nchini akitokea nchini Canada majira ya saa sita mchana na moja ya mambo atakayofanya katika msafara huo ni pamoja na kuzindua matawi katika jimbo la Arumeru mashariki na Arusha mjini na baadaye atafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Relini jijini Arusha.
"Kuanzia majira ya saa 12 asubuhi watu wataanza safari ya kuelekea uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro KIA na watamsubiria mgeni wao hadi saa sita mchana atakapowasiri."
Mungure alitoa kijembe kwa wabunge waliopora ubunge akiwemo mbunge wa Arusha mjini, wakae mkao wa kufungasha kwani mwenye jimbo Lake amerejea.
Baadhi ya wafuasi wa chadema akiwemo kada maarufu wa ccm,maarufu kwa jina la Jumapili walipongeza ujio wa Lema wakidai wamejipanga kumpokea bila kujali itikadi zao za vyama na kwamba ujio wa wake katika jimbo la Arusha mjini utakuwa na taswira chanja ya kuchochea maendeleo kwani ni mbunifu na mkosoaji asiye na woga.
"manufaa makubwa waliyoyakosa wakati Lema akiwa ugaibuni nchini Canada.
Lema kwa takribani miaka mitatu alienda kuishi ujamishoni kwa kile kinachoelezwa ni changamoto za kisiasa,hivyo ujio wake unatazamwa kuleta mageuzi ya kisiasa katika jimbo la Arusha mjini.
0 Comments