TEKNOLOJIA YA TEHAMA YA KUWAKWAMUA VIJANA KIUCHUMI YAJA RUSHA


Na Joseph Ngilisho Arusha 


WADAU wa Tehama mkoani Arusha wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha uwepo wa kituo cha ubunifu wa Tehama kinachotarajiwa  kujengwa  mkoani Arusha hivi karibuni. 


Akizungumza katika ufunguzi  huo leo jijini Arusha Kaimu Katibu Tawala msaidizi Daniel Loiruck amesema kuwa uwepo wa kituo hicho utaongeza chachu kubwa kwa vijana katika kuendeleza bunifu zao kupitia Tehama na kujulikana kimataifa zaidi.




Amesema kuwa ,uwepo wa vituo hivyo utasaidia sana    kuibua vituo vya ubunifu kwa vijana kutoka katika halmashauri Ili  kufungua fursa zakiuchumi kupitia Tehama.


Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Tehama Dr Nkundwe  mwasaga amesema kutokana na uchumi wa kidigitali kukua  Afrika ,wameanza na mikoa 5 ilikuifanya Tanzania kua na vijana shindani katika kuyafikia masoko makubwa nakutumia bunifu zao kukuza uchumi .



Nao baadhi ya wabuni wameomba ujezi wa vituo  kiharakishwe kwa kanda ya kaskazini Ili vijana kupata ujuzi na kukuza bunifu zao.





Ends....

Post a Comment

0 Comments