TBA YAWANG'OA WADAIWA SUGU ,YUMO MPANGAJI ANADAIWA MILIONI 30


Na Joseph Ngilisho ,Arusha 

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Arusha ,imeanza operesheni  ya kuwaondoa wapangaji ambao ni  wadaiwa sugu ndani ya nyumba zake ,kutokana na malimbikizo ya kodi  yanayofikia kiasi cha zaidi ya sh,milioni 130 .

Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo,akiwemo mdaiwa sugu mwenye malimbikizo ya zaidi ya sh, milioni  30,kaimu meneja wa TBA mkoa wa Arusha ,Mhandisi Juma Dandi alisema kuwa operesheni hiyo ni ya nchi nzima na imelenga kukusanya fedha za serikali.


Alisema kuwa zoezi hilo linalenga kutoa wapangaji wasiozingatia mikataba yao ya upangaji hususani katika ulipaji  kodi ya pango.

"Tunaowapangaji wengi ambao wengi wao ni watumishi wa serikali lakini miongoni mwao wachache wamekuwa wakorofi ,hawazingatii mikataba yao ya upangaji wa nyumba tumekuwabtukiwapa nosti za kusudio la kuwaondoa lakini bado wanakaidi "

Alisema awali waliainisha wapangaji wapatao 38 mkoa wa Arusha  wenye  malimbikizo ya kodi ya muda mrefu, lakini baadhi yao walilipa na kubakia na wapangaji wachache ambao  TBA imefikia uamuzi wa kuwatoa kupitia dalali wa mahakama wa kampuni ya udalali ya Twins Auction Mart Co LTD ya mkoani Rukwa.




Kwa upande wake dalali wa mahakama aliyepewa zabuni ya kukusanya madeni hayo kupitia kampuni hiyo , Zuberi Lumbizi alisema kuwa mahakama imewapa jukumu la kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu wa TBA nchi nzima na tayari mikoa sita nchini wameshaipitia.


Alisema changamoto wanayokumbana nayo wakati wa kutekeleza zoezi hilo ni kukuta nyumba zimefungwa lakini kupitia viongozi wa mtaa wanaoambatana nao,hulazimika kuvunja milango na kutoa vitu nje chini ya uangalizi wa viongozi hao wa mtaa.

"Tunapomtoa nje ya nyumba mpangaji tunamwachia vitu vyake ila sisi tunafunga nyumba yetu"

Ends.....







Post a Comment

0 Comments