PICHA :TAZAMA MAMIA WALIVYOZIMIA WAKIAGA MIILI 12 YA MAREHEMU WA FAMILIA MOJA... DC LUSHOTO ,RC K/NJARO WASHINDWA KUVUMILIA

 


Na Joseph Ngilisho, ROMBO 


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameongoza mamia ya waombolezaji wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro, kutoa heshima za mwisho kwa miili 12 kati ya 14 ya familia moja waliofariki kwa ajali mkoani Tanga huku ndugu na jamaa wakishindwa kujizuia na kuangua vilio na baadhi yao kuzimia .

Hata hivyo majeneza hayo hayakuruhusiw  kufunguliwa ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kuaga Sura za wapendwa wao kutokana na miili hiyo kuharibika .


Ajali hiyo ilitokea Februari 4,  katika eneo la Magira Gereza, wilayani Korogwe, barabara ya Segera - Buiko na kusababisha vifo vya watu 21 mpaka sasa wakati gari aina ya Fuso lilipogongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya Coaster lililokuwa likisafirisha mwili wa marehemu ,ndugu na majirani.

Ndugu hao pamoja na majirani walikuwa  wakisindikiza mwili wa ndugu yao, Athanas Mrema (59) aliyefariki dunia Februari Mosi, kutokea jijini Dar es Salaam kuja mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko ndipo walipopata ajali hiyo mbaya.


Akiongea katika hafla ya kuaga miili ya merehemu ,iliyofanyika katika viwanja vya hospitali ya kanisa katoliki ya Huruma,mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Nurdin Babu alisema msiba huu ni mkubwa hauwezi kuelezeka kwani familia na mkoa  zimepoteza nguvu kazi ya Taifa.
Jeneza jipya la mwili wa MAREHEMU Athanas Mrema aliyekuwa akisafirishwa kutoka Dar es laam



Alisema mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo februali 4 mwaka huu ,rais Samia suluhu Hassan alitoa pole kwa familia zilizopotelewa ndugu zao na kuagiza taratibu za mazishi zifanywe na serikali.

"Jana majira ya saa tano usiku miili ya marehemu ilipokelewa mkoani Kilimanjaro na itazikwa Rombo , Himo na Kilema na Katika mazishi ambayo yanafanyika leo, ipo familia moja ambayo inazika watu watano kwa wakati mmoja, familia nyingine wawili pamoja na wengine ambao wanazikwa mwili mmoja mmoja. "


Aidha mkuu huyo wa Mkoa alitoa raia kwa viongozi wa dini kuzidisha maombi makanisani na msikitini ili kuepusha ajali kama hiyo zisiweze kutokea tena.

Aliwataka madereva wa magari kuzingatia  umakini barabarani ili kuepusha ajali zisizo na ulazima.


Naye mkuu wa wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga,alisema msiba huo ni mkubwa na umepoteza nguvu kazi ya taifa.


Alilitaka jeshi la polisi hapa nchini kuongeza jitihada za kuwabana madareva wasiozingatia  sheria za usalama barabarani hasa nyakati za usiku na kuwachukulia hatua kali.

Alisema tangia siku ya tukio ajali ilipotokea yeye akikaimu wilaya ya Korogwe,usiku na mchana walikuwa akipigania kuokoa  majeruhi na kukwamua marehemu waliokuwa wamenasa kwenye mabaki ya magari hayo yaliyosabajisha ajali hiyo.


Hata hivyo alidai kusikitishwa na kuongezeka kwa majeruhi wengine wanne waliokiwa wamwlazwa wakipatiwa matibabu na kufikia marehemu 21 jambo alilowataka watanzania kuzidisha maombi kuwaombea marehemu waliobaki waweze kupona haraka.

Katika viwanja hivyo vilio vilitawala na baadhi yao kuzimia wakati wa kutoa heshima za mwisho katika  miili hiyo iliyokuwa kwenye majeneza 12 likiwemo la Athanas Mrema aliyefariki jijini Dar esalaam februali 1 mwaka huu.


Miongoni mwa marehemu hao ipo familia moja imepotez watu 14 ambapo baadhi yao wanatarajiwa kuzikwa leo.

Ends..




Post a Comment

0 Comments