MWENYEKITI WA HALMASHAURI LONGIDO MATATANI ATAKIWA KUJIUDHULU..YEYE ARUKA FUTI 100


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido, SIMON OITESOI ameingia kwenye mgogoro wa kiuongozi na kutakiwa kujiudhulu kufuatia kushindwa kusimamia mamlaka yake ipasavyo katika baraza la madiwani na kuruhusu upotevu wa mamilioni ya pesa za halmashauri hiyo kunakofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.


Katika kikao kilichoketi cha baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo,mwenyekiti huyo alionekana kuwa busy na simu wakati kikao  kikiendelea jambo linalotazamwa kama ni utovu wa nidhamu kwa mkuu wa wilaya  MARKO NG'UMBI aliyekuwa akitoa maelekezo ya serikali. 

Baadhi ya madiwani walidai kuwa ulegevu wa mwenyekiti umelikosesha MENO baraza hilo kiasi cha kushindwa kuhoji matumizi mabaya ya fedha yanayosababishwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo.

Katika baraza hilo mkuu wa wilaya alilieleza baraza hilo la madiwani jinsi baraza hilo limeshindwa kusimamia mapato ya halmashauri huku fedha nyingi zikipotea bila kuwepo usimamizi .


Alisema makusanyo ya halmashauri hadi desemba mwaka jana yalifikia zaidi ya bilioni 1.036 lakini hadi sasa ni sh,milioni 90 pekee zimeenda kwenye maendeleo na hiyo ni chini ya asilimia 7 tu ambayo ni kinyume na utaratibu unaozitaka halmashauri kutoa asilimia 40 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

"Mlitakiwa angalau mmetoa sh,milioni 414 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Longido ,ukimya wako mpaka sasa unamaanisha  nini kama wewe sio sehemu ya haya madudu yanayiendelea hapa"

Ndani ya kikao hicho mkuu hiyo wa wilaya hakupepesa macho pale alipoeleza wazi kuwa halmashauri hiyo imejaa upigaji.

Alisema kuwa fedha zinazotokana na mapato ya halmashauri zinapigwa kabla  hazijaingia kwenye mfumo unaotakiwa kwa kutumia mashine za POS(fedha Mbichi).

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo,Simon Oitesoi alipohojiwa kwa njia ya simu alidai kwamba yeye sio legevu kama anavyozushiwa ila amefanya jitihada kubwa kupitia kamati ya fedha na baraza la madiwa kusimamishwa kwa viongozi sita wa halmashauri hiyo.

Alisema kuwa viongozi waliosimamoshwa kupisha uchunguzi ni pamoja na Afisa mapato wa halmashauri hiyo,Afisa biashara,Injinia ,afisa Manunuzi.

Alisema watumishi hao ambao wamesimamishwa miezi miwili iliyopita na nafasi zao kukaimishwa, wanatuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha ,kupitia leseni za biashara ambapo wamekuwa wakikusanya mapato bila fedha hizo kupitia kwenye mfumo wa serikali.

"Mimi sihusiki na chochote na hizo tuhuma zinazozushwa, ni kwamba hata mkuu wa wilaya hakutamka hayo maneno ni baadhi ya watu ndio wanazusha kutokana na sababu zao wenyewe "

Alisema anajiandaa kutoa taarifa juu ya hatua zilizochukuliwa mara baada ya mkaguzi wa ndani kutoa taarifa yake na kwamba ikibainika walihusika watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Ends....






Post a Comment

0 Comments