Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kanda ya Kaskazini kimedai kuwa maandalizi ya kumpokea aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbress Lema hapo kesho yamekamilika, ambapo maelfu ya wananchi, viongozi wandamizi wa chama hicho akiwemo mgombea urais nchini Kenya Prof. George Wajackoyah watakuwepo.
Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha, katibu wa chadema kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema ujio wa Lema utaenda sambamba na kufungua matawi katika maeneo ya Tengeru, Kikatiti wilayani Arumeru na Ilboru mkoani Arusha.
Alisema atatua uwanja wa ndege Kia majira ya saa sita mchana hapi kesho na baadaye atasindikizwa na mamia ya wafuasi wa chana hicho kuelekea mjini Arusha kwa ajili ya kuongea na wananchi juu ya yaliyomsibu hadi kuondoka nchini Tanzania katika viwanja vya relini jijini hapa.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Dini na siasa watakuwepo akiwepo Askofu Mwamakula, na wajumbe wa Chama hicho kutoka bara na Visiwani.
Alisema ujio huo unatarajiwa kupokelewa na wazazi wa Lema katika uwanja wa ndege Kia akiwa na familia yake akirejea nchini kutoka nchini Canada baada ya kukaa ugenini kwa zaidi ya Miaka miwili kwa kile kinachodaiwa misikosuko ya kisiasa iliyotishia maisha yake na familia yake.
Hivi Karibuni alirejea nchini makamu mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lisu na kulakiwa na maelfu ya wananchi ambapo hivi sasa shauku ya wengi ni kumuona tena Lema ambaye amekuwa akibebwa na hisia za wengi kutokana na utashi wake wa Siasa.
Naye Prof. George Wajackoyah
alidai kuwa yeye ndiye aliyeshiriki kumtorosha Lema kutoka mikononi mwa Askari wa Kenya katika mpaka wa Namanga na Nchini Kenya na kwenda kumpatia hifadhi kabla ya kwenda nchini Canada.
Pamoja na mambo mengine prof, Wajackoyah alisema amekuja Arusha kushuhudia demokrasia na anamoongeza rais Samia suluhu Hassan kwa maendeleo makubwa katika kipindi kifupi cha uongozi wake
"Nilimnyakua Lema mikononi mwa polisi na kufanikiwa kumvusha nchini Kenya sikuogopa kufa na hadi sasa siogopi kufa"
"Nilitokwa na machozi baada ya kumwona Lema mzalendo wa kweli akipambania taifa lake "
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha Prof. Wajackoyah alimwagia Lema sifa za ukomavu wa Siasa na kusema hajawahi juta kumfahamu Lema.
"Nilipambana kumsaidia Godbless Lema kutokana na maisha yake kuwa hatarini kisiasa na nikafanikisha kuwasiliana na mashirika mbalimbali ya haki za Binadamu Amnesty na mengine kuhakikisha Lema anapata hifadhi nchini Canada lakini pia kumtoa mikononi mwa Polisi wa Kenya waliotaka kumrejesha Tanzania" alisema.
Alisema anamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu kuruhusu mikutano ya siasa na kuita kuwa hiyo ndio demokrasia ya kweli.
Alidai kuwa amekuja kushuhudia ujio wa Lema ambaye amekuwa nchini Canada kwa miaka zaidi ya Miwili sasa na kwamba alifurahishwa na maamuzi ya kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara nchini Tanzania.
Ends...
0 Comments