Na Joseph Ngilisho ARUMERU
Mwili wa Mzee Emmanuel Mollel(78) ambaye ni Baba wa mfanyabiashara maarufu wa Madini Mkoa wa Arusha na Manyara umezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Marurani wilayani Arumeru Mkoani Arusha huku maelfu ya wakazi ndugu na jamaa wakijitokeza kumlilia Marehemu.
Akiongea katika mazishi hayo,Joel Saitoti ambaye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watano wa marehemu alisema baba yake aliwalea katika maisha mazuri yenye upendo na na furaha, nasasa ameondoka watamkumbuka daima.
Saitoti ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa kampuni za uchimbaji madini za Tanzanite Azo Africa Limited na Germ and Rock Ventures alisema amempoteza mtu muhimu katika maisha yake na ataendelea kumkumbuka daima kwa ukarimu na ucheshi wake na hana budi kumshukuru mungu kwa yote.
Alisema marehemu baba yake alikuwa nguzo muhimu ya mafanikio yake ila anamshukuru mungu na kuahidi kuendelea kumwombea huko aliko.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa serikali,wananchi wachimbaji wa madini zaidi ya elfu tatu walishiriki kwenye mazishi hayo kutokana na umaarufu wa mfanya biashata huyo pamoja na marehemu baba yake.
Baadhi ya wafanyabiashara wenzake waliojitokeza katika msiba huo wamesema kwamba marehemu alikuwa nguzo ya maisha na wamepoteza mtu muhimu kati ya wazee ambao walikua ni msaada mkubwa sana katika kijiji hicho.
Katika msiba huo maelfu ya waomborezaji walikula , kunywa na kusaza na mazishi hayo kusindikizwa na mvua kubwa ambayo ilisimama kwa muda mrefu .
Ends...
0 Comments