LILIPOFIKIA JENGO REFU ARUSHA NI MAKAO MAKUU YA PAPU AFRIKA,WAZIRI NAPE : LITAWEKA ALAMA ARUSHA

 


Na Joseph Ngilisho,Arusha


JENGO la mradi wa Makao makuu ya Umoja wa Posta, Afrika (PAPU), linalojengwa kwa ubia wa nchi ya Tanzania na PAPU jijini Arusha, huenda likakamilika ifikapo Aprili mwaka huu baada ujenzi wake  kufikia asilimia 94.4 ya mradi huo hadi sasa .

Hayo yamebainishwa na msimamizi , mshauri wa mradi, Mhandisi ,Hanington Kagiraki wakati waziri wa habari,mawasiliano na Teknolojia ya Habariz Nape Nnauye alipotembelea uwekezaji huo unaogharimu kiasi cha sh, bilioni 47 hadi kukamikika ikiwa hadi sasa kiasi cha sh,bilioni 35 zimeshatumika.

Akiongea mara baada ya kutembelea jengo hilo lenye urefu wa gorofa 18, waziri ,Nape Nnauye amezitaka taasisi zinazotoa Huduma za maji na umeme kuongeza kasi zaidi  jengo la Umoja wa Post Afrika (PAPU)liweze kukamilika kwa wakati na kuleta taswira na madhari nzuri kwa Jiji la Arusha


Alisema serikali  ya Tanzania imetoa asilimia 40 ya gharama za ujenzi huo kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) huku asilimia 60 ya gharama za ujenzi huo zinatoka kwa nchi wanachama wa PAPU

"Jengo hili litakamilika Aprili mwaka huu na naaagiza watoa huduma za maji na umeme kuharakisha huduma hizo mara moja ili kuwezesha jengo hilo kuwa la kisasa zaidi"

Alimpongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuendeleza mradi huu ulioasisiwa na watangulizi wake, kuhakikisha jengo hilo linajengwa nchini Tanzania na kuwa Makao Makuu ya PAPU na kusisitiza kuwa jengo hilo litakuwa linatoa huduma za posta kidigitali zaidi .


"Mradi huu umeanza muda mrefu na unachangiwa na wanachama wote wa posta afrika kwa asilimia 60 huku nchi ya Tanzania ikiwa mbia wa mradi huo kwa kuchangia asilimia 40 hadi kufikia mwezi wa nne mwishoni mradi utakuwa umekamilika"

Naye Katibu Mkuu wa PAPU,Dk,Sifundo Chief Moyo alisema umoja huo kujengwa nchini Tanzania ni fahari kwa nchi hiyo sanjari na wanachama wengine kwani utaongeza chachu ya kusukuma mbele maendeleo ya utoaji huduma za haraka kwa nchi za Afrika.

Huku Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema ujenzi wa jengo hilo utawezesha mkoa kunufaika kiuchumi ikiwemo fursa mbalimbali za mikutano 

Ends...

Post a Comment

0 Comments