JUBILEE YA MIAKA 50 YA MLIMA KILIMANJARO USIPIME ..TANAPA YAJIPANGA KUUJULISHA UMMA KUWA NI MALI YA TANZANIA

 


Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa TANAPA,linatarajia kufanya maadhimisho ya kwanza ya  miaka 50 tangia kuanzishwa kwa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro yatakayofanyika, Machi 16 Mwaka huu katikq makao makuu ya mlima huo yaliyopo, Marangu Mkoani Kilimanjaro .

Akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha,naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho  alisema maadhimisho hayo  ya kwanza ya aina yake , yanalenga pia kuutambulisha umma kuwa mlima huo  unapatikana katika nchi pekee ya Tanzania.


Alisema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Marangu, mkoani Kilimanjaro, huku Makamu wa Rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni Rasmi. 

Alisema maadhimisho ya  jubilee ya miaka 50 ya mlima Kilimanjaro ni utaratibu wa kawaida wa Tanapa na hii ni baada ya kufanya maadhimisho kama hayo ya miaka 60 ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti. 


"Kilele cha Mlima kilimanjaro kitafanyika Marangu Mkoani Kilimanjaro  yalipo makao makuu ya Mlima huo huku makamu wa rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni rasmi "

Alisema mlima huo wenye urefu wa kilometa 5,895 ulianzishwa rasmi kama hifadhi ya Taifa Kilimanjaro , Machi 16, Mwaka1973 kwa ajili ya shughuli za utalii. 

"Tunataka kuihakikishia dunia kwamba mlima Kilimanjaro upo eneo la Tanzania na kuonyesha maendeleo ya utalii kwa mlima Kilimanjaro tangu hifadhi ilipoanzishwa na hadi leo hii tunafikia  miaka 50 tumepita katika vipindi mbalimbali vya utalii," alisema Batiho.

Naye kamishna  msaidizi wa  hifadhi,Angela Nyaki ,alisema k maadhimisho hayo yataanza Machi 1,hadi kilele machi 16 mwaka huu,na mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo usafi wa Mlima utakaofanyika kwa siku kumi kuanzia machi 1,ambapo wadau wa utalii wapatao 500 watashiriki.


Alisema shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe za maadhimisho hayo  ni pamoja na ugawaji na upandaji wa miti, zoezi litakalozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.

"Pia tutawatembelea waongoza utalii wa miaka ya 70 ili kuzungumza nao na kupata uzoefu wao na ushauri wao"

Alisema tangu kuanzishwa kwa shughuli za utalii katika mlima Kilimanjaro, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo ongezeko la watalii na kufikia elfu 50 kwa mwaka, kuongezeka kwa njia za kupandisha mlima huo kutoka njia moja hadi kufikia njia sita .

Ends.  




Post a Comment

0 Comments