DKT SLAA RASMI CHADEMA!,APANDA JUKWAA LA CHADEMA ,ATAKA MAPAMBANO YA KUDAI KATIBA MPYA YAENDELEE


BY NGILISHO TV  


Aliyewahi kuwa Katibu wa Chadema Taifa na b­aadaye Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbroad Slaa kwa mara ya kwanza jana Jumapili amehudhuria mkutano wa Chadema Wilaya ya Karatu na kuahidi atashirikiana na chama hicho kudai Katiba mpya.

Dk Slaa aliondoka Chadema akiwa Katibu Mkuu wakati wa mchakato wa uchaguzi Mkuu mwaka 2015 baada ya chama hicho, kumteua Edward Lowassa kugombea urais kupitia chama hicho.

Miaka takriban minane baada ya kuondoka Chadema, jana Dk Slaa amepanda katika jukwaa la Chadema Wilaya ya Karatu ambako awali alianzia harakati zake za kisiasa.

Dk Slaa alikuwa Mbunge wa Karatu kwa kwa miaka10 kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 na  tangu alipotangaza kujiondoa Chadema alikuwa hajapanda kwenye jukwaaa la Chadema.

Hata hivyo, jana Dk Slaa amepanda Jukwaa la Chadema kuwasalimia wakazi wa Karatu katika Kata ya Rhotia ambapo kulikuwa na mkutano wa Chadema.

Katika mkutano huo ambao ulikuwa unajadili mambo kadhaa ikiwepo mgogoro wa maji katika mji wa Karatu, Dk Slaa alipopata muda wa kuzungumza alieleza sera nzuri za Chadema.

Alieleza harakati kadhaa za Chadema kusaka dola na kueleza anaimani chama hicho kimekomaa sasa kushika dola.

Dk Slaa pia ameahidi kushirikiana na Chadema  kudai Katiba Mpya kwani ameeleza Katiba inachangia kero nyingi za wananchi.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Wakili Samweli Welwel Akizungumza na Mwananchi Digital leo 27, 2023, amesema Dk Slaa walimpa fursa kuzungumza na wananchi wa Rhotia ili awasalimie.

Welwel amesema chama hicho kimemualika wilayani Karatu Dk Slaa kuhudhuria kikao cha wadau wa maji ambacho kitafanyika leo.

Kikao hicho kinatokana na Uamuzi wa Serikali kuvunjwa Bodi ya Maji ya Karatu mjini na Vijijini (Kaviwasu) na kuunda bodi mpya ya Maji.

Amesema hata hivyo bado chama hicho hakijampokea rasmi kurudi chadema kama ambavyo imeanza kuonekana baada ya kuzungumza na wananchi wa Karatu.

Amesema kama kuna hoja za kumpokea Dk Slaa Chadema suala hilo litafanywa na viongozi wa kitaifa, lakini hadi sasa Dk Slaa amezungumza hatakuwa katika siasa za moja kwa moja katika vyama vya kisiasa.

Post a Comment

0 Comments