Na Joseph Ngilisho Arusha
Familia zenye watu zaidi ya 300 katika mtaa wa Olevolosi Kata ya Sinoni jijini Arusha hazina mahala pa kuishi mara baada ya kundi la watu zaidi 80 wakiwa na Sururu , nyundo na shoka, kuvamia nyumba zao na kubomoa makazi yao likiwemo gorofa linalofikia thamani ya sh, milioni 100.
Tukio hilo limetokea mapema leo majira ya asubuhi na kuzua taharuki kubwa kwa wananchi na wakazi hao wasijue la kufanya kutokana na mgogoro wa Ardhi uliokuwepo, kumalizika mahakamani na kumpa ushindi
Luis Kawishe aliyekuwa na mgogoro na wakazi 11 wa eneo hilo.
Akiongelea tukio hilo diwani wa kata ya Sinon ,MICHAEL KIVUYO alisema ameshtushwa na tukio hilo akidai kwamba uongozi wa kata na mtaa haukushirikishwa ili waweze kuwaelimishq wananchi na kuepusha athari ambazo zingeweza kujitokeza
Baadhi ya waathiriwa wa tukio hilo ,Saluni Laizer na Ramadhan Gendo walisema kuwa utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa haukufuata utaratibu ikiwemo kusudio la kuwaondoa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo,Adrian Mswata alisema ameshangazwa na utekelezaji wa zoezi hilo kwani hadi sasa haelewi ni amri ya mahakama imetolewa au la, kwani wao kama viongozi wa mtaa huo hawakushirikishwa juu ya uvunjwaji wa nyumba hizo zaidi ya 10.
0 Comments