Na Joseph Ngilisho Arusha
Viongozi wa dini mbalimbali katika jiji la Arusha wanatarajia kushiriki dua maalumu ya kumwombea Rais Samia Suluhu Hasani inayoandaliwa na taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa itakayofanyika januari 28 mwaka huu katika viwanja vya msikiti mkuu wa ijumaa jijini hapa.
Akiongea na vyombo vya habari ,msemaji wa taasisi hiyo sheikh Haruna Husein amesema kuwa dua hiyo itaongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela ambaye atakuwa mgeni rasimu wa tukio hilo.
Amesema kuwa tukio hilo la kipekee hapa nchini,limelenga kumwomboa rais Samia kwa kuendelea kudumisha amani ya taifa h,pia kuomba mvua ambayo imekuwa ikisuasua na hivyo kutishia kuwepo kwa changamoto ya chakula kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.
Katika hatua nyingine KIONGOZI huyo wa dini amempongeza rais Samia kwa kufanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi ya wilayani kwa kuteua wakuu wapya wa wilaya na wengine kuwabadilisha vituo vya kazi.
Alisema kuwa baadhi ya wakuu wa wilaya wanapoteuliwa wamekuwa mizigo kwa kushindwa kwendana na kasi ya rais Samia ikiwemo kuwahudumia wananchi ndio maana amefanya mabadiliko haya na kuwaondoa kabisa baadhi yao alioona hawaendani na kasi yake.
Katika mabadiliko hayo rais Samia amewateua wakuu wa wilaya wapya 37 akiwemo Felisian Mtehengerwa aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arusha na kupangua wengine 48 kwa kuwabadilishia vituo vya kazi akiwemo Saidi Mtanda aliyehamishiwa wilaya ya Urambo mkoani Tabora akitokea wilaya ya Arusha.
Ends..
0 Comments