Na Joseph Ngilisho Arusha
MKUU wa mkoa wa Arusha, John Mongela,amewataka wakuu wapya wa wilaya Mkoani humo, kuacha mihemko ya kukimbilia kuwakamata wananchi na kuwaweka ndani badala yake wajifunze kuongoza bila kutumia vyombo vya dola.
Aidha amewapongeza waliokuwa wakuu wa Wilaya za ,Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango na mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe ambao wamestaafu utumushi wao bila kuwa na uongozi wenye mihemko
Kauli hiyo ameisema wakati akiwaapisha wakuu wapya, Felician Gaspar Mtahengerwa(Arusha),Emmanueli Kaganda(Arumeru), Suleiman Mwenda (Monduli)ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida,na Marko Mumbo, (Longido), ambao waliteuliwa wiki iliyopita
Alisema kuwa wakuu hao wa Wilaya wanapaswa kufuata kanuni na sheria za utawala wa kisheria na kujitenga na utawala wa kutumia mabavu na vyombo vya dola.
"Mnaniona mimi sina tabia ya kuweka ndani wananchi kama kuna mmoja wenu hapa anyooshe mkono ,yapo makosa ya kuweka watu ndani ,naomba mkafanye kazi kwa hekima na kwa mujibu wa sheria na msiwe wavivu wa kutaka ushauri"
Alisema "hakuna kitu cha kishamba kinaniuzi kama kiongozi kuropoka ropoka"
Aidha alisema kuwa viongozi wallop sio bora zaidi kuliko wengine ambao hawajapata nafasi hizo hivyo watekeleze majukumu yao kwa kuwa nafasi hizo ni nzuri iwapo watatumia hekima na busara zaidi katika utendaji wao vinginevyo inaweza zikawa ni mbaya
Mongela,amewataka wasiwe ni watu wa kuropoka ropoka kwani huo ni ushamba waache kutoa maagizo yasiyo tekelezeka bali watumie hekima wawe mahiri katika kutekeleza majukumu watoe maelekezo na kuyasimimia
Alisema hapendi tabia ya kukamata watu na kuwaweka mahabusu,Viongozi wa aina hiyo wamepungikuwa sifa za Uongozi,wakamate tu pale inaposhindikana
Kuhusu wanafunzi,amewataka wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia wanafunzi wote kuanzia msingi hadi sekondari wanaenda shuleni na katika hilo hakuna kubembelezana wachukue hatua kwa yeyote atakaeshindwa kumpeleka mtoto shule
Akitoa nasaha zake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha,Stivini Zelothe,amesema kuwa nchi yetu ina rasilmali ya kutosha ya Viongozi na haina upungufu lakini watu wote hawawezi kuwa Viongozi na chama kinawategemea wakafanye kazi waliyopewa wakatekeleze Ilani ya CCM,kwa vitendo.
Aliwataka wasipandishe mabega bali wawe wanyenyekevu kwa wananchi,na kila jambo litakalotokea wahakikishe wanatumia buasra waheshimu watu na kuongeza kwamba wapo baadhi wakishapewa madaraka wanajisahau
Aliwataka wakashirikiane na Viongozi wengine waliopo wasiende kuanzisha mapambano ,kwenye Chama kuna Kamati ya maadili wakawasikilize wananchi wasiwe ni miungu watu,wondoe vikwazo vya kuwaona yaani appointment
Alisema Chama hakina mzaha mwakani ni uchaguzi wa serikali za mitaa na Chama cha mapinduzi kitaenda kunadi sera kwa wananchi hivyo hakiingii kwenye uchaguzi huo kwa maneno bali kwa vitendo.
Ends...
0 Comments