Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
Nabii Mkuu wa kanisa la ngurumo ya upako Dkt David Kasambale( Geordavie) ameiomba serikali kuanza kuchunguza na kuyadai kodi makanisa yanayouza visaidizi kama maji ,mafuta ,chumvi,udongo ,juice wakiwaminisha waumini kwamba vinaponya wakati hakuna ukweli wowote.
Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika ibada ya jumapili wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo ambapo alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya makanisa ambayo viongozi wake wamekuwa wakitumia visaidizi kuwadanganya waumini na mbaya zaidi wamekuwa wakitumia mgongo wa kanisa kufanya biashara mbalimbali huku wakitumia njia ya makanisa kutokulipa Kodi ya Serikali.
Alibainisha kuwa ni vyema kanisa likabaki ni mahali pa kutoa na kufundisha neno la Mungu na sio sehemu ya kufanya biashara kama baadhi ya viongozi wa dini wanavyofanya biashara za kuwauzia waumini visaidizi kama mafuta ,chumvi ,juice sabuni na vinginevyo huo ni utapeli.
"Nipende kuwaambia tu baadhi ya viongozi wa dini kama nguvu ya Mungu ipo ndani yako itabaki nguvu za mungu na kanisa litaendelea ata ukifiatilia kwenye vitabu vyetu vya dini hakuna sehemu ambayo inasema Yesu aliuza mafuta ,maji Wala chumvi katika kipindi chake ,Wala hakuna Mahali Yesu aliwakusanya watu wakafa kisa kugombania mafuta ,niseme tu wanaofanya hivyo nimatapeli tu hivyo ni vyema watu wakaamka wakasimama kwenye msingi wa zamani ambao ni neno la Mungu "alisema nabii Mkuu Dkt Geordavie
Alibainisha kuwa wakati umefika kwa watanzania na waumini kuachana na visaidizi na warizike na nguvu za mungu wanayohubiriwa na wachungaji wao
"Niwatake tu viongozi wa dini ambao wanauza visaidizi hivyo wawe wafanyabiashara wa kawaida kama wameamua kuwa wauza maji na walipe kodi ya serikali kama inavyotakiwa na wasitumie mgongo wa kanisa kukwepa kodi ya serikali "alibainisha
Alisema kuwa iwapo serikali itawaachia hawa viongozi wakaendelea kufanya vitu hivi ipo siku maafa makubwa yanaweza kutokea kwani hata maafa yaliyotokea katika baadhi ya nchi yaliyotokana viongozi wa dini kuwasanganya waumini wao
Aidha pia aliwataka viongozi wa dini mbalimbali kuwahudumia waumini wao kimwili na kiroho ambapo alifafanua kuwa kiroho ni kuwalisha neno la Mungu ,kimwili ni kuwasaidia waumini wao katika swala zima la mitaji ili kuweza kuwakwamua katika umaskini ambapo alisema Kwa kufanya hivyo watakuwa wame hata Rais wa nchi yetu dkt Samia Suluhu kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.
Ends..
0 Comments