NABII MKUU GEORDAVIE AMWAGA MAPESA SOKO LA SAMINGE

 


Na Joseph Ngilisho,Arusha


KIONGOZI Mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako Nabii Mkuu  Geor Davie ametoa hundi ya sh,milioni 100 kwa ajili ya kusaidia wajasiriamali wa  soko la Samunge lililopo  Jijini Arusha ili waweze kujikwamua kiuchumi baada ya soko hilo kuungua miaka mitano iliyopita na kuteketeza mali zao.


Aidha amewaomba viongozi wengine wa dini kutoa  sehemu ya mapato yao ya sadaka  na kuwasaidia wananchi wenye uhitaji kwa kuwa  wamekuwa wakitoa sadaka kwa kujinyima ili hali ,hali zao za maisha ni duni.


 

Akikabidhi mfano wa hundi ya sh, milioni 50 aliyokuwa ameiandaa kabla ya kuongeza kiasi kama hicho nankufikia milioni 100,alisema amepokea maombi kupitia viongozi wa soko la samunge kuhusu mahitaji ya wafanyabiashara wadogo,hivyo amewiwa kuwachangia sh,milioni 100 huku mbunge Mrisho Gambo alichangia sh,milioni 10.




Alifafanua kuwa kati ya fedha hizo sh,milioni 80 inaenda kwa watu wenye uhitaji wafanyabishara hao huku sh,milioni 20 zikiingia katika ukarabati huo wa soko hilo.


Nabii huyo mkuu ambaye ni Balozi wa Amani alisema neno amani halina dini na aliomba wananchi wamuunge mkono Rais Dk,Samia Hassan Suluhu.



Naye mbunge wa arusha Mjini mrisho Gambo alichangia sh,milioni 10 na kuonya fedha hizo zitumike kama ilivyokusudiwa na ziwafikie walengwa akiahido kufuatilia kwa ukaribu watu watakaonufaika na fedha hizo.

Kupitia risala ya uongozi wa soko hilo iliyosomwa na Loviness Damas walimwomba nabii mkuu ,kuwa mlezi wa soko hilo kwa sababu limekuwa la hali ya chini kwa muda mrefu ,hatua ambayo nabii mkuu aliikataa ombi hilo akidai anamajukumu mengi ya kichungaji



Alisema alipokea barua ya kuomba msaada katika soko hilo na alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo kwakutoa ahadi ya sh,milioni 10  katika soko hili.



Alishukuru kwakuwa mlezi wa soko hilo ingawa hata weza ulezi wa moja kwa moja na atashirikiana nao kwa kila hatua.


Ends.... 

Post a Comment

0 Comments