MWENYEKITI UWT ARUSHA AMSHUKIA VIKALI MBUNGE MAGIGE, AMTAKA AACHE DHARAU NA PESA ZAKE..TUTATUMIA KALAMU YA 200 KUMKATAA

 


Na Joseph Ngilisho Arusha 

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake (UWT)CCM Mkoa wa Arusha, Flora Zelothe amemjia juu Mbunge wa Viti maalumu mkoani humo, Catherine Magige(ccm) kwa kufanya ziara na kugawa misaada bila kufuata utaratibu akidai hizo ni dharau zilizopitiliza.

Akiongea kwenye kikao cha Baraza la UWT Meru,wilaya ya Arumeru, mwenyekiti huyo alidai kuwa mbunge huyo bado anaendekeza makundi ndio maana ameshindwa kujeshimu uongozi wa UWT na kufuata utaratibu wa chama katika kutekeleza majukumu yake jambo alilodai hatalifumbia macho.


"Haiwezekani Mwenyekiti wa UWT mkoa apange ziara na imeingia kwenye vikao na yeye anakuja alikotoka anaanza kutoa maelekezo upya bila kufuata utaratibu hii ni dharau iliyopitiliza"

"Kama sio busara zangu ziara aliyofanya mbunge kwenye wilaya yangu ni madharau makubwa ,kutokuniheshimu na imelenga kunidhalilisha"

"Mkoa wa Arusha ni maarufu sana kwa wanaccm kuendekeza makundi inataka uwe na moyo mpana ,masikio mapana mdomo mdogo, lakini uwe na ngozi ngumu kama yangu"


Akiongea huku akinukuu kanuni za chama hicho kuhusu kazi za wabunge alisema"Nitapokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi za wabunge ,wawakilishi ,Viti maalumu iliyoandaliwa na kamati ya utekelezaji na kutoa mapendekezo ya taarifa hiyo kwenye kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la UWT Taifa "

Zelothe alisisitiza kuwa maana halisi ya kibengere hicho ni kwamba  wabunge wote wa ccm Mkoa wanawajibika chini ya ofisi ya UWT mkoa.


"Kwa msingi huo Magige alipofanya ziara Arusha mjini na Meru tuliamua kukaa kikao na kukubaliana kwamba tumwache  wamalize ziara yao lakini baadaye tuwaite ,tusemezane nao na watakaopo tukataa ,tutatumia kalamu  ya shilingi miambili ,tutawakataa"

"Na mimi nilimwambia mwenyekiti wa UWT Meru amwache  awape wanawake chakula ,awape nauri,alete na propaganda na alete na vitendea kazi vya kumalizia jengo letu la mashine kwa sababu ni majukumu yake ila tatizo hapa ni utaratibu haukufuatwa"

Alisema mbunge huyo anawajibika katika  ofisi ya UWT mkoa ,kamati ya utekelezaji na sio shotikati za kwenda kwenye wilaya kwa kutumia mabavu na mihemko ya pesa zake.

Ends...




 


Post a Comment

0 Comments