Na Joseph Ngilisho,Arusha
Mfanyabiashara Maarufu wa Utalii Mkoani Arusha na Mkazi wa Ngaramtoni ,Francis Temba anashikiliwa na polisi kwa madai ya kuwabaka watoto wake wanne huku akiwatishia kwa bastola.
Kabla ya kuwabaka Watoto wake hao wa Kike MfanyabiasharaTemba alikuwa akiwalazimisha Kwa kuwatisha Kwa silaha aina ya bastola ili atimize malengo yake ya kuwabaka na alifanikiwa kufanya hivyo Kwa nyakati tofauti akiwa nyumbani kwake Ngaramtoni Arumeru .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishina Msaidizi wa Polisi,Justin Masejo alipoulizwa juu ya kuwepo Kwa tukio hilo alisema hana taarifa rasmi ila aliahidi kulifuatilia na kulitolea taarifa.
"Kwa Sasa Sina taarifa rasmi ila ngoja nifuatilie halafu ntakupa Taarifa"alisema Masejo kwa kifupi.
Habari kutoka Kituo cha Polisi Usa River zilidai kuwa mmoja wa watoto hao wa kike{jina tunahifadhi} alifungua malalamiko jalada USR/RB/4415/2022 katika kituo hicho desemba 3 mwaka huu.
Vyanzo wa kutoka Polisi na familia ya watoto hao wa kike zilidai kuwa watoto wengine watatu hawakufungua jalada la malalamiko na hiyo ni baada ya kupatiwa maelezo polisi kuwa mtoto mmoja akifungua inatosha na binti aliyefungua alitoa maelezo yote polisi Usa.
Mmoja wa wanafamilia alidai kuwa kuibuka kwa sakata hiyo ni kufuatia watoto hao wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 19 hadi 23 wa mama tofauti kwenda mjini Moshi na kuwalalamikia wazazi wao juu ya Baba yao mzazi kuwafanyia unyama huo.
Alisema baada ya taarifa hiyo kuwafikia wazazi wa watoto hao waliamua kwenda ofisi ya kata ya Ustawi wa Jamii na kueleza hilo na maofisa hao waliwashauri kwenda ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kilimanjaro{RCO} na walifanya hivyo.
Mtoa taarifa huyo alidai walipofika ofisini kwa RCO Kilimanjaro na kueleza yaliyowakuta aliwaelekeza kufungua kesi Arusha kwa kuwa tukio hilo limefanyika Mkoani Arusha.
Alisema wazazi hawakukata tamaa walifanya hivyo kwa tarehe tajwa hapo juu katika Kituo cha Polisi Usa River na kupewa jalada la namba USR/RB/4415/2022 na mtuhumiwa alikamatwa na kuhojiwa na kusalimisha silaha aliyokuwa akiwatishia watoto wake na kuwabaka bila ridhaa yao.
Hata hivyo baadhi ya wazazi wa watoto hao wameonekana kushikwa na butwaa na kushindwa kujua kinachoendeleaa kwani kesi imefunguliwa muda mrefu hakuna taarifa wanayopewa na kibaya zaidi mtuhumiwa amerudishiwa silaha yake.
‘’Tunaomba viongozi wa juu wa serikali na jeshi la polisi kuliangalia hili kwani mzazi anabaka watoto kwa nguvu huku akiwawekea bastola pembeni kichwani ili atimize malango yake lakini naona kuna dalili zote za rushwa’’alilalamika mmoja wa wazazi wa kike wa watoto hao
Habari za ndani toka polisi Usa zinadai kuwa tukio hilo limewagawa polisi kwani wengine wanalalamika baadhi yao kuchukua rushwa na kuficha jalada na wengine wanasema ni uzembe mkubwa kesi hiyo kuwa polisi kwa muda wote bila kwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe.
Vyanzo vya habari vilidai kuwa mmoja wa Kigogo wa Polisi Usa River ndio anayemlimba mfanyabiashara Temba na inadaiwa amechota mzigo wa kutosha kuhakikisha anamlinda mfanyabiashara huyo asishitakiwe.
Habari zaidi zilidai kuwa kitendo cha watoto kuripoti polisi kimetafsiriwa vibaya na upande wa wazazi wa Baba na kudai kuwa nguvu ya ziada inafanyika kuzima kesi hiyo kwa kuwatisha watoto iwapo watakuwa na msimamo huo hawatapelekwa chuo.
Vyanzo viliendelea kusema kuwa vikao vya kifamilia vimekuwa vikikaa mchana kutwa na usiku mnene bila mafanikio ila polisi ndio wenye kusimamia vikao hivyo ili kutimiza malango yao.
Ends..
0 Comments