MAPESA YA NABII MKUU GEORDAVIE YAPAGAWISHA WAFANYABIASHARA SAMUNGE ..AKABIDHI MILIONI 100 ALIZOAHIDI..MWENYEKITI AHOJI MABILIONEA WA TANZANITE WAPO WAPI


Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 


HATIMAYE Nabii Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako,  GeorDavie, amekabidhi rasimi  hundi ya sh,milioni 100 aliyoahidi  kwa wafanyabiashara wa soko la Samunge jijini Arusha na kuibua shangwe kwa wafanyabiashara hao waliojikusanya kushuhudia hundi hiyo.


Nabii GeorDavie alitoa ahadi hiyo januari 23 mwaka huu katika soko hilo, baada ya kupokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara hao juu ya uhitaji kutokana na kuunguliwa kwa soko hilo miaka minne iliyopita na kupoteza Mali zao .


Akikabidhi mfano wa hundi hiyo kwa mwenyekiti wa wafanyabiashara kwa niaba ya Nabii mkuu GeorDavie,katika hafla iliyofanyika katika soko hilo,
 msaidizi wa Nabii, Balozi ,Sekela Ntondolo aliwataka wafanyabiashara hao kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.

"Leo nimekuja kukabidhi fedha hizo sh,milioni 100 alizoahidi nabii mkuu na nitakabidhi na nakala ya malipo ya benki inayoonesha fedha hizo tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti ya wafanyabiashara wa soko la Samunge"


Awali mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo Njola Miraji, alimshukuru nabii mkuu kwa kutimiza ahadi yake akidai kuwa wapo mabilionea waliotokana na madini ya Tanzanite lakini wameshindwa kusaidia  jamii yenye uhitaji .

Alisema katika fedha hizo wameorodhesha majina ya  wafanyabiashara 1261watakaonufaika na fedha hizo na tayari majina hayo ameyakabidhi kwa nabii mkuu kama alivyoelekeza wakati akiajidi fedha hizo . 



Naye mkuu wa soko hilo,Restituta Nyoni aliwataka wafanyabiashara watakaonufaika na fedha hizo kuzielekeza kwenye biashara husika na kuepuka kuzipeleka mambo yasiofaa ikiwemo kwenye vikoba.

"Endapo utapokea hizo fedha nenda kafanye biashara usiende kunywea pombe au kuingiza kwenye vikoba"


Baadhi ya wafanyabiashara hao wakiwemo wadau wa maendeleo akiwemo, Max Akyo walimshukuru nabii Mkuu GeorDavie kwa moyo huo wa huruma na ukarimu wake na kuwataka wafanyabiashara na watumishi wengine wa mungu kuiga mfano huo ili kuisaidia jamii yenye uhitaji.


Wafanyabiashara hao wametakiwa kufungua akaunti binafsi za  benki, ili kuwezesha fedha hizo kutumwa moja kwa moja kwenye akaunti zao.

Ends..

Post a Comment

0 Comments