KISHINDO CHA BENKI YA UBA ARUSHA,YAFUNGUA TAWI KATIKATI YA JIJI ,WAFANYABISHARA WAPAGAWA


 Na Joseph Ngilisho,ARUSHA


BENKI ya United of Afrika (UBA) imezindua Tawi Lake jipya la nane katika jijini Arusha,na kuwataka wafanyabiashara kuchangamikia fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu kwa lengo la kukuza biashara zao.

Akiongea wakati  uzinduzi wa tawi la benki hiyo iliyopo katika kata ya Levolosi mkabala na Ofisi ya Shirika la nyumba la taifa (NHC),Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Lawrence Mafuru,kwa niaba ya Waziri wa fedha na Mipango dkt.Mwiguli Nchemba aliitaka benki hiyo kuongeza  uwekezaji nchini kutokana na ukubwa wa benki hiyo.


Mafuru alisema kuwa benki hiyo ni kubwa katika bara la Afrika  na Dunia kwa ujumla hivyo ni vema uwekezaji ukaongeza katika bara la Afrika kulingana na ukubwa wa benki hiyo.

"Kwanza niwapongeze  kwa hatua ya kuongeza tawi hapa mkoani Arusha  lakini ukubwa wa benki yenu ni mkubwa sana mwaka jana niliona ni dola bilioni 27 za marekani,hivyo mna jukumu la kuongeza uwekezaji uendane na benki yenu"Alisema Mafuru


Aidha alizitaka taasisi zote za fedha  kuendelea kuboresha huduma za fedha  kwa kuwa ni sekta muhimu ila inakuwa taratibu  kwa asilimia  chini ya kumi.

Alisema kuwa zipo njia nyingi za kukuza sekta hiyo ikiwemo kuongeza huduma hizo karibu na wanachi na kufungua matawi katika maeneo ya vijijini ili wanachi wahifadhi fedha zao kwa usalama.

Akisoma kwa risala  kwa niaba ya mwenyekiti  wa bodi ya benki hiyo ni ,Martin Mmari alisema benki hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ikiwemo sekta ya Elimu na Afya kupitia UBA Faundation.

Pia alisema kuwa jumla ya vijana wa kitanzania 200 wamenufaika na mikopo ya ukuzaji wa biashara zao.

Naye Mkurugenzi wa UBA Tanzania Gbenga Makinde maarufu kama GMak  alisema kuwa benki hiyo imejiwekea malengo ya kuhudumia wafanyabiashara katika bara la Afrika na ina matawi nane sasa.


Matawi hayo ni Dar es salaam manne,Dodoma,Rufiji,Mwanza na Arusha,huku mpango ukiwa ni kusogeza huduma katika mikoa mingine ambayo ni Mbeya,Zanzibar,na Mtwara. 

Awali meneja wa benki hiyo Wiliam Kiwale,alisema ujio wa UBA katika Mkoa wa Arusha unalenga kuwakomboa wafanyabiashara kutokana na mikopo ya riba nafuu .


Alisema riba ya benki hiyo ipo chini ukilinganisha  na mabenki mengine na kuwataka wafanyabiashara kuchangamikia fursa hiyo ili kujikwamua kiuchumi na kukuza biashara zao.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhulia uzinduzi huo,Prosper Msofe na Godfrey shirima walisema ujio wa benki hiyo ni fursa kwa wananchi hususani wafanyabiashara na kuipongeza benki hiyo yenye mtandao mkubwa duniani


"Wafanyabiashara wasiogope kukopa kwani kukopa ndio njia sahihi ya kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla"alisema shirima".


Ends..



Post a Comment

0 Comments