ARUMERU:KIJANA AUAWA KWA KUCHAPWA FIMBO ZAIDI YA 250


Na Joseph Ngilisho ARUMERU 

KIJANA Nelson Mollel (32) mkazi SANAWARI wilayani wa Arumeru Mkoani hapa,amefariki dunia baada ya kuchapwa fimbo takrinani 280 akimtuhumiwa kumtukana mama yake mzazi matusi ya Nguoni.


Wazee wa jamii ya Kimaasai na Kimeru wilayani Arumeru mkoani Arusha wamekuwa wakitoa adhabu ya kuwachapa viboko 70 kwa vijana ambao wamekuwa wakibainika kufanya matendo yanayokwenda kinyume cha maadili Yao.


Miongoni mwa matendo hayo ni pamoja na kutukana wazazi, kunywa pombe mchana na kufanya vurugu, kuvaa nguo ambazo sio za heshma na kufanya uhalifu ikiwepo kupigana.

Mama mzazi wa marehemu ,  Janeth Kimario  amesema kwamba kijana wake alimtukana Matusi ya nguoni  siku ya tarehe moja mwaka mpya 2023 na baadaye kumwambia baba yake mdogo Abel Mboya (45)  ambaye alimwita na kumpeleka porini na kuanza kumchapa fimbo 70 .

 
Mama mzazi wa marehemu amesema  adhabu aliyo pata mwanae ni kubwa sana na ni kweli alistaili kuchapwa kwa kufundishwa adabu   pia waandishi niseme tu kwamba awajaniambia mimi adhabu itakua kubwa kiasi cha kumpoteza mwanangu alisema mama wa marehemu “

Pia mama wa marehemu amesema mara baada ya tukio ilo baba mdogo wa marehemu  alisha wai kumpiga yeye  na kumvunja kidole na kumwambia bado atafanya mauaji kwa wengine iwe fundisho .

Kwa upande wake Enjo Isaya  ambaye Marehemu ni Mjomba wake amesema tukio ilo ni ukatili sana hivyo serikali ichukue atua kwa wausika.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Arumeru Eng Richard Ruyango amesema wanafahamu utaratibu wa kutolewa kwa adhabu za fimbo 70 lakini kilicho fanyika ni zaidi ya adhabu ya fimbo 70 hivyo ni tukio la mauaji hivyo serikali itawachukulia atua kali walio usika na mauaji ayo


Post a Comment

0 Comments