Na Joseph Ngilisho Arusha
AFISA Elimu Mkoa wa Arusha Mwl. Abel Ntupwa amesema, hadi sasa ni asilimia 56.5 ya wanafunzi 23,023 waliyo jiunga na elimu ya kidato cha kwanza katika mwaka wa masomo 2023 huku lengo kuu likiwa ni wanafunzi 40,288 katika mkoa wa Arusha.
Ntupwa alisema kuwa mwitikio huo ni mkubwa katika wiki ya kwanza ya masomo toka shule zifunguliwe, Jan 9,2023 huku akiwataka wazazi na walezi kuwapeleka wanafunzi mashuleni ili waweze kuendelea na masomo.
Afisa elimu huyo alieleza kwamba Rais Dkt Samia Suluhu hassan alitoa kiasi cha shilingi Bilion tano ili kuhakikisha vyumba vya madarasa vinajengwa na kukamilika kwa wakati katika shule zote za umma zipatazo 268 za Mkoa wa Arusha.
"Niwasihi wazazi wote wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa na kupangiwa shule wanawapeleka mapema maana masomo yameshaanza na waache mila potofu ambazo hazina faida katika jamii zetu ambazo zinapelekea mtoto kukosa elimu". aliongeza Ntupwa.
Aidha katika hatua nyingine Afisa elimu huyo aliwapongewa wanafunzi waliyofutiwa matokeo ya darasa la saba na kisha kurudia mitihani yao na kufaulu kwa asilimia 100 hii ni kuonesha wazi kwamba wanafunzi hao waliiva vizuri.
Shule yenye mchepuo wa kiingereza ya Kilimanjaro English Mediam pamoja na shule ya High Charange ni shule zilizokumbwa na kadhia ya kufutiwa matokeo ya darasa la saba katika mkoa wa Arusha kutokana udanganyifu .
Hata hivyo uongozi wa shule ya Kilimanjaro Medium umeipongeza serikali kwa hatua zote walizo fikia hadi kuwapa watoto haki yao ya msingi ya kufanya mtihani wa marudio na kisha kuwapangia shule kwaajili ya kuendelea na elimu ya sekondari.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo, Piniel Hando, aliishauri serikali kuhakikisha inapanga wasimamizi wa mitihani waminifu hatua itakayosaidia kuepukana na udanganyifu wa mitihati unaosababishwa na baadhi yao wasio waaminifu.
"Kwanza niwashukuru wazazi tuliweza kuungana nao kwa kipindi chote hadi serikali ilipotoa mitihani ya marudio kwa wanafunzi wetu pia niwapongeze wanafunzi kuwa na utulivu na uvumilivu mkubwa na hatimaye kufanya mtihani hiyo ya marudio Alisema Hando.
Aidha Hando aliwatoa hofu wazazi kwa kueleza kwamba shule hiyo ya Kilimanjaro imejipanga vyema katika utoaji wa elimu bora na yenye kukidhi viwango vya kimataifa na kitaifa pia imepanga vyema kuhudumia wanafunzi katika malezi bora yanayo weza kukuza uelewa na vipaji vyao.
Alieleza kwamba katika mwaka wa masomo 2023 shule hiyo imepokea watoto wapatao 120 kwa ajili ya elimu ya awali(Chekechea), huku darasa la kwanza wakijunga hadi sasa ni 65 ,na hii ni kuonesha kwamba wazazi bado wanaimani kubwa na shule yao.
Mmoja ya wanafunzi waliorudia mitihani hiyo ,Hayrath Yusufu ameishukuru Serikali kwa kuruhusu kurudia mitihani kwani hapo awali walijiona kama wamepoteza muda wao bure wa miaka saba kukaa darasani iwapo kama wasingerudia mitihani yao.
Ends..
0 Comments