Na Joseph Ngilisho Arusha
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax, amewasihi wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kuendeleza mtangamano ili kukuza biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Alisema suala hili ni muhimu kwani lazima kwenda pamoja katika sekta mbalimbali hususani programu za kuendeleza miundombinu inayoakisi uchumi wa kijiografia.
Dkt Tax aliyasema hayo jana jijini hapa katika hafla ya kuwaapisha wabunge wapya wa EALA,ambapo wabunge wote waliapa na kuahidi kupigania masl
ahi ya wananchi wa nchi wanachama.
ahi ya wananchi wa nchi wanachama.
Alisema changamoto za ulinzi na usalama pia lazima zishughulikiwe ipasavyo ili nchi za EAC ziwe na amani.
Naye makamu wa rais mstaafu wa Kenya ,Kalonzo Musyoka aliwataka wabunge wa EALA kusimamia usawa ulioanzishwa na waasisi wa jumuiya hiyo ikiwemo kufungua mipaka na kuwa na sarafu moja kwa nchi wanachama.
"Kujiunga kwa nchi ya DRC kwenye Jumuiya, kuna msukumo mkubwa kwa upande wa uchumi, hivyo nijukumu la wabunge wa EALA kuimarisha usawa,kuondoa changamoto zilizopo na kufungua mipaka na kuwe na sarafu moja iliyokuwepo zamani"alisema.
Wabunge wa Tanzania waliochaguliwa na kuapishwa katika bunge la EALA ni Angela Kizigha, Dk Shogo Mlozi, Dk Abdullah Makame, Machano Ali, Mashaka Ngole, Ansar Kachambwa, James Millya, Dk Ngwaru Maghembe na Nadra Mohammed.
Katika hafla hiyo, pia spika wastaafu wa EALA akiwemo Abdulrahman Kinana, Martine Ngoga na Margareth Zziwa walikuwepo.
Mmoja wa wabunge kutoka Tanzania walioapa wakiongozwa na Katibu wa EALA, Alex Obarti, James Millya, aliomba Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo katika nchi za EAC.
Millya aliwataka Watanzania kuamka na kutumia fursa mbalimbali zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Alisema atahamasisha Watanzania waweze kuchangamkia fursa hizo.
"Nipo tayari kutembea kwenye vyuo vikuu na maeneo mengine nchini kwa ajili ya kuhamasisha mazingira mazuri ya uwekezaji, kwani ndani ya EAC kuna fursa mbalimbali haswa katika kilimo na huduma nyingine"
Millya aliongeza atakuwa balozi mzuri wa kuisemea Tanzania na EAC kila mkoa ili kutangaza fursa zilizopo EAC.
Alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa kuaminiwa kuwa miongoni mwa wabunge hao kutoka Tanzania na kuongeza kuwa, atahakikisha kila fursa za kibiashara anazitumia.
Ends..
0 Comments