UWT MOSHI MJINI YAJA NA MPANGO KABAMBE KUKABILI UKATILI ... SERIKALI KUWAUNGA MKONO..

 


Na Gift Mongi M
oshi


Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Moshi Mjini Theresia Komba amesema zipo programu mbalimbali za kimichezo  zilizoandaliwa kwa ajili ya wanawake na wasichana ambazo zimelenga kuwainua kiuchumi na kuwawezesha  kukabiliana na aina yoyote ya dhuluma, manyanyaso, ukatili na ubaguzi.


Komba ametoa kauli hiyo mjini hapa mbele ya naibu waziri wa utamaduni Sanaa na michezo Paulina Gekul aliyekuwa mgeni rasmi katika bonanza  la michezo lililoandaliwa na shirika la kuwezesha wanawake(Florida  women empowerment) kushirikiana na umoja wa wanawake Tanzania wilaya ya Moshi Mjini lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha michezo nchini.

 


Aidha amesema wanawake wanatakiwa kuunganishwa kwa njia mbalimbali kama michezo fursa za kiuchumi lakini pia kuwajengea uwezo wa fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


"Sisi kama UWT Moshi Mjini tumejipanga kwa mambo mbalimbali yakumwezesha mwanamke ili aweze kujikwamua na hili tamasha la leo  ni njia mojawapo ya kuwaweka sehemu moja ili tuweze kuzungumza lugha moja yakusonga mbele"amesema

 


Kwa upande wake Gekul amezitaka halmashauri zote  katika mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha zinatenga fedha kwaajili ya uendeshaji wa michezo ili  kuhakikisha viwanja pamoja na vifaa vya michezo vinapatikana. 


Aidha amezitaka serikali za mitaa kuhakikisha wanakuwa  na maeneo kwa ajili ya michezo ili kukuza vipaji vya watoto pamoja na vijana pamoja na kuimarisha afya kupitia michezo




"Ili kuendelea kuimarisha sekta ya michezo, viongozi kuanzia serikali za mitaa wanapaswa kuhakikisha wanatenga maeneo ya michezo,  kuyalinda yasivamiwe na kuyaendeleza ili kuwasaidia wananchi na kukuza vipaji vya watoto pamoja vijana"amesema


Bonanza hilo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete ,kuvuta kamba,, kukimbia na magunia kufukuza kuku,kukimbia na yai kwenye kijiko, mdako, mchezo wa kuruka kamba huku washindi wakikabidhiwa zawadi mbalimbali  na kusindikizwa na  burudani kutoka kwa wasanii wa  mkoani hapa.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments