TAZAMA PICHA UKATILI WA KUTISHA MAMA AMCHOMA KAMA NYAMA MTOTO WA KUMZAA,INASIKITISHA

 



 

Na Joseph Ngilisho,ARUSHA

MTOTO mwenye umri wa miaka 7 mkazi wa Kitongoji cha Kitiengare,Kimandolu,jijini Arusha,amelazwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru akiugulia maumivu makali mara baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kuunguzwa na pasi ya moto na mama yake mzazi,Dorice Lema akimtuhumu kuchelewa kumfungulia mlango.

Aidha kufutia tukio hilo,wananchi wenye hasira kali walijikusanya na kutishia kuvamia kituo cha polisi cha baraa wakitaka mtuhumiwa aliyekuwa amekamatwa atolewe  ili wamshughulikie.



Akieleza ukatili huo ,mtoto huyo(jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la kwanza ambaye amejeruhiwa sehemu za mgongoni , makalioni  ,mapajani na alama za kung'atwa na meno ,aliiomba serikali imchukulie hatua kali mama yake ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

"Naiomba serikali imchukulie hatua kali mama yangu kwani ananitesa sana".


Alisema siku ya tukio mama yake alimwacha nyumbani na kumfungia ndani na aliporejea majira ya saa mbili usiku alijaribu kugonga mlango mara kadhaa bila kufunguliwa baada ya mtoto kupitiwa usingizi na baadaye aliposhtuka na kufungua mlango ndipo mama yake alipo mshika mkono na kumvutia ndani na kuchukua pasi na kuichomeka kwenye umeme na kuanza kumuunguza kama nyama sehemu mbalimbali za mwili.

Kwa upande wake diwani wa viti maalumu,kata hiyo, Rafa Mollel pamoja mtoto mwenye  nyumba aliyopanga mtuhumiwa wasimulia kwa masikitiko namna mama huyo alivyotekeleza tukio hilo la kikatili na kusema kuwa mama huyo anapaswa kuchunguzwa akili kwani licha ya kumtaka aeleze sababu za kushambulia mwanaye wa kuzaa kwa pasi ya moto alikuwa akijibu kwa mkato,nisamehemi.
Diwani Rapha Mollel 




"Huyu mama tangia apangishe hii nyumba ya mama yangu hana mwezi mmoja ila kila siku saa kumi na moja alfajiri lazima umsikie huyu mtoto analia akipigwa na siku ya tukio mama yake baada ya kumchoma na pasi alimfungia ndani"

"Siku hiyo tulisikia kelele mtoto akilia kwa nguvu na kesho yake hatukumwona akiongea wala kutoka nje ,ndipo mimi nilipoamua kukaa kimya ndani kwangu na baadaye mama huyo alipoona watu wote hawapo alitoka ndani na kwenda kwenye shughuli zake na ndipo na mimi nilipotoka kwangu na kwenda katika chumba chake kuangalia kama huyo mtoto yupo, ndipo nilimwona akiwa amesimama, hawezi kukaa wala kulala ,alikuwa na  majeraha makubwa ya moto,niliita jirani na baadaye tukaenda kwa  balozi ambaye alituambia tuende kutoa taarifa polisi"


Alisema wananchi walipobaini tukio hilo walijikusanya hadi kituo cha polisi cha baraa na kutaka mtuhumiwa afungukiwe ili wamshughulikie lakini baada ya hali kuwa mbaya magari mawili ya polisi kutoka mjini Arusha yalifika na polisi kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao waliokuwa na hasira kali.

Ends..



Post a Comment

0 Comments