TAZAMA MAMIA YA WANANCHI WAKIGOMBEA KUPANDA MABEHEWA MAPYA YA TRC,DC MTANDA AMSHUKIA KIGWANGALA

 


Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

KUWASIRI  kwa mabehewa mapya 16 ya shirika la reli nchini TRC katika jiji la Arusha,kumeibua shangwe kwa wakazi wa jiji hilo ambao wameipongeza serikali na kueleza namna mabehewa hayo yatakavyo saidia punguza changamoto ya usafiri katika mikoa ya kanda ya kaskazini na mikoa mingine nchini. 

Wananchi hao walifurika pasipo kujali mvua iliyokuwabikinyesha  katika viwanja vya TRC jijini hapa kushuhudia ujio wa mabehewa hayo mapya ya aina yake ,ambapo pamoja na kuishangilia treni iliyokuwa na mabehewa 11 yakiwemo matano yaliyokuwa yakipakia Mkoani Kilimanjaro.


Walipata fursa ya kupanda ndani ya mabehewa hayo na kujionea viti vya kisasa,vyumba vya kulala mke na mume au familia ,sehemu ya kula na kunywa na vyoo vya kisasa .

Pamoja na hayo wakati Treni hiyo  ikiondoka jijini ARUSHA ,majira ya saa 8.30 mchana wananchi walionekana  kugombea kupanda ndani  ya mabehewa hayo tayari kwa kuondoka kuelekea dar kupitia mikoa ya mbalimbali. 


Treni hiyo ikiwa na  mabehewa  mapya iliwasiri jijini hapa majira ya saa sita mchana na  kupokelewa na mkuu wa wilaya ya Arusha Saidi Mtanda, ambaye aliwaonya baadhi ya wananchi yanayoyabeza akidai kwamba wanapotosha umma kwa maslahi yao binafsi.

"Mtu anayeuguza mgonjwa ndiye anayejua anasumbukiwa na nini hao wanaoyaponda mabehewa yetu hawana jema niwakupuuza"


Awali kaimu mkurugenzi TRC nchini,Focus Sahani alisema kuwa mabehewa hayo ni sehemu ya mabehewa  22 mapya yaliyonunuliwa na serikali nchini Korea na kuwataka wananchi kutumia usafiri wa tren kwa sababu mabehewa hayo ni ya kisasa na yenye huduma zote muhimu ikiwemo za starehe ya kulala ,kula na kunywa na huduma za simu.


Naye meneja wa kituo cha Treni Arusha,Vickta Ngingo alisema , usafiri wa treni katika mkoa wa Arusha ni msaada mkubwa kwa wananchi na  utakuwa ukifanyika mara tatu kwa wiki ,jumanne alhamis na jumamosi na katika madaraja yote matatu bei zake ni nafuu. 


Post a Comment

0 Comments