TAZAMA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ATC )KINAVYOIBUA VIPAJI KWA WANAFUNZI WA SEC.
Na Joseph Ngilisho Arusha
TUME ya Sayansi na Teknolojia ya vyuo vikuu COSTECH,imekipongeza Chuo kikuu cha Chuo cha ufundi Arusha,kwa kuanzisha program maalumu ya mafunzo ya ubunifu,biashara na ujasiriamali kwa wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Arusha ili kuwawezesha kuibua miradi itakayowawezesha kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Ndaki ya Costech,dkt .Erasto Mlyuka kutoka Costec,alipokuwa akitunuku vyeti kwa wanafunzi na walimu wa shule hizo waliofanya vizuri katika wiki ya mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali wakati wakiwasilisha miradi yao ya ubunifu,katika hafla iliyofanyika chuo cha ufundi Arusha ATC.
Alisema kupitia Programu hiyo ya Future Stay Busness (FSBL)wanafunzi wameonyesha umahili katika kuandaa ubunifu wa miradi ya kiuchumi ambapo wakimaliza shule watakuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki biashara zao.
"Mfumo wa Programu ya FSBL ni mradi unaolenga kuwasaidia wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi na unafanyika nchi nzima lengo ni kuwajenga uwezo wanafunzi kufanya bunifu wakiwa mashuleni na mwanzo wa safari ya mafanikio"alisema
Programu hiyo inashirikisha walimu, wanafunzi na wafanyabiashara ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakiwaongoza na kusimamia ubunifu wa miradi husika inayoibuliwa ambapo wanafunzi hao hutumia taaluma yao ya kuwa bidhaa na biashara kwa kuzingatia kanuni za kisayansi.
Mlyuka,alisema Programu hiyo ilianzishwa mwaka 2017 katika chuo kikuu cha Dar es Salaam,kwa kushirikisha shule tano za sekondari , na sasa ipo katika chuo cha ufundi Arusha ambapo hushirikisha shule saba ikiwa ni kutanua program hiyo ambayo inalenga kuzifikia shule zote za sekondari nchini.
Aliongeza , Programu hiyo inawawezesha wanafunzi hao kuelewa changamoto za ajira na biashara na hivyo wao kupata suluhuhisho ambapo wanakuwa na uwezo mkubwa kuanzisha miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo viwanda pindi wakihitimu elimu
Awali mkuu wa Chuo cha ufundi Arusha, Dkt.Mussa Chacha, alitoa wito kwa shule za sekondari mkoani Arusha hasa zenye mchepuo wa Sayansi kutembelea chuo hicho ili kujifunza jinsi somo la Phiyzikia linavyofanya kazi kwa vitendo
Alisema matatizo makubwa duniani ni maarifa sahihi ya kufanya jambo kwa vitendo hivyo akashauri wanafunzi wapewe maarifa sahihi ili wayatafsiri katika vitendo na kuwawezesha kubuni na kuibua miradi ya kiuchumi.
Naye makamu mkuu wa Chuo hicho mhandisi, Yusufu Mhando,alisema mafunzo ya ubunifu yatawawezesha wanafunzi kuwaongoza kwenye ujasriamali na kuwa wabunifu kwenye biashara zao na hivyo kuboresha maisha amewaomba watembelee chuo hicho kwa kuwa ni taasisi ya maarifa
"Wanafunzi wa kike wenye sifa tunawakaribishwa kujiunga katika chuo chetu cha ufundi Arusha ili waweze kuendeleza vipaji vyao "
Shule zilizoshiriki ni Arusha Girls ,Arusha sekondari, Iliboru, Edmund rise,St Mary iliyopo Duluti , St Jude na Bishop Durning ambapo shule ya wasichana ya Arusha girls High school iliibuka kidedea ikifuatiwa na shule ya sekondari ya Arusha huku Ilboru ikishika nafasi ya tatu.
Ends...
0 Comments