Na Joseph Ngilisho Arusha .
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya rufaa iliyofunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watano.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Desemba 14, 2022 na Jaji Salma Maghimbi ambaye anasikiliza shauri hilo,⁷ baada ya jana kusikiliza hoja za pande zote mbili.
Jana mawakili wa Sabaya na wenzake watano wameweka pingamizi la awali katika kesi ya rufaa waliyofunguliwa na Serikali.
Hata hivyo kesi hiyo imepangwa kutajwa desemba 21,2022 ,pia mahakama hiyo imeagiza warufaniwa wanne namba 2,3,5 na namba 7 .
Warufaniwa hao ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya kuandikiwa wito wa kufika mahakani kupitia vyombo vya habari ambayo ni magazeti yenye wasomaji wengi zaidi.
Kwa mujibu wa sheria za mahakama warufaniwa hao wasipotokea mahakamani kesi hiyo itaendelea kusikilizwa upande mmoja na watakosa hakinyao ya msingi ya kuwaailisha utetezi wao
0 Comments