Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
Serikali imemkatia rufaa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya na wenzake watano kupinga kuachiwa huru katika kesi ya uhujumu uchumi,iliyotolewa JUNI 10,mwaka huu.
Juni 10,2022 Sabaya na wenzake sita walishinda kesi ya uhujumu uchumi na kuachiwa huru baada ya mahakama hiyo kubaini ushahidi uliotolewa na Jamhuri ulighubikwa na utata hivyo kushindwa kuthibitisha mashitaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani.
Sabaya alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,ambapo mahakama hiyo ilipanga kuanza kusikiliza rufaa hiyo iliyokatwa na upande wa Jamhuri dhidi ya Hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,kuanzia kesho desemba 13 mwaka huu.
Mbali na Sabaya wajibu rufaa wengine ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021 iliyotolewa uamuzi na mahakama hiyo aliyekuwa mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo (Watson Mwahomange) hajajumuishwa katika rufaa hiyo.
Mbele ya Jaji Salma Maghimbi, Sabaya alifikishwa mahakamani hapo huku Serikali ikiwakilishwa na mawakili wa Serikali waandamizi Patrick Mwita, Abdallah Chavula, Hebel Kihaka, Felix Kwetukia na Timotheo Mmari.
Kwa upande wake Sabaya, aliieleza mahakama kuwa hana mwakilishi na amepata wito wa mahakama leo na hakujua anakuja kufanya nini mahakamani hapo .
Sabaya ameiomba mahakama hiyo wiki mbili ili aweze kujiandaa na kufanya mawasiliano na mawakilimawasiliano na mawakili wake pamoja na familia yake.
"Mheshimiwa naomba unitendee haki nahitaji wiki mbili kujiandaa kwani nina appointment na madaktari KCMC tarehe 15, na kuna mipangilio ya malipo kwa mawakili naomba unipe muda ili haki itendwe kikamilifu," Sabaya.
Baada ya maelezo hayo Jaji huyo alimweleza Sabaya kuwa rekodi zinaonyesha aliachiwa huru na Jamhuri imekata rufaa.
Kwa upande wake wakili Mwita, ameieleza mahakama kuwa kesi imepangwa kwa ajili ya kusikilizwa na hati ya wito mahakamani ilitolewa Desemba Mosi mwaka huu.
Jaji Maghimbi aliahirusha shauri hilo na kusema kuwa rufaa imepangwa kusikilizwa mfululizo kwa muda wa siku tano na wakili wa Sabaya hajatoa taarifa yoyote kwa mahakama hivyo rufaa hiyo inaanza kusikilizwa hapo kesho.
Ends
0 Comments