GAMBO ASHUSHA TUHUMA NZITO,ADAI VIONGOZI WA SERIKALI WANATAKA KUMUUA,WAMWEKEA KONDOMU MBICHI NYUMBANI KWAKE

 


Na Joseph Ngilisho Arusha 

MBUNGE wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ameibua tuhuma nzito dhidi ya viongozi wa serikali akiwatuhumu kumvamia nyumbani kwake mara mbili wakitaka kumuua kwa sumu akidai kuwa amelazimika kuishi kama digidigi.

Pia amedai kuwa watu hao baada ya kuvamia nyumbani kwake, kupekua na kumkosa waliacha kondomu mbichi iliyotumika  ili ionekane kwamba alikuwa anachepuka na mwanamke mwingine nje ya ndoa.

"Hawa watu wameishiwa wamepambana kunipa sumu wameshindwa kwa sababu mimi sio lofalofa mimi hata nikienda mahala naenda na maji yangu,watakachoweza ni kunivizia getini kunipiga risasi" 


Hayo aliyabainisha jana wakati akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika soko kuu la Arusha,  akidai kuwa watu hao walimvamia mara mbili nyumbani kwake kwa lengo la kutaka kumuua.

"Hao watu walionivamia ni watu wa  serikali na wengine nawajua ipo siku wakinikamata nitaona rangi zote"


Hata hivyo Gambo hakufafanua lengo la watu hao kumvamia na kutaka kumtoa roho na hakueleza iwapo aliwahi kutoa taarifa kituo cha polisi juu ya madai hayo.

Gambo ambaye aliwapiga marufuku wanaccm kuvaa sare zao katika mkutano wake alidai kuwa hawezi kutishwa na mtu yoyote na yupo tayari kuitwa mahala popote akajieleze na haogopi kuwa mbunge wa awamu moja.

Katika hatua nyingine Gambo alishusha tuhuma zingine nzito kuwa kuna vikundi vitano vimelipwa milioni 100 bila kuidhinishwa na halmashauri, alivitaja vikundi hivyo kuwa ni Furahia,Chapakazi ,Esajo ,Bulunga na Mashu , wizi mtupu.

"Rais Samia  alisema tengeni fedha mkawakopeshe kina mama na vijana lakini watu wanakwenda kuchepusha na kupeleka vikundi ambavyo wanamaslahi navyo mambo haya mimi siwezi kukubali ,hata kama nitakuwa mbunge wa awamu moja nitahakikisha nawanyoosha sawasawa"

Aliongeza kuwa kuna vikundi vingine vimepewa sh,milioni 830 wamekwenda kutumia kwenye matumizi yao binafsi hawakufanya biashara yoyote,waambieni waache utani na fedha za umma. 

"Wametumia milioni 36 matumzi yake hayaeleweki kabisa,wametumia milioni 580 matumizi yake hayaeleweki wakataja kuna wazabuni tumewapelekea vifaa,wazabuni walipoitwa kila mtu alisema hafahamu chochote ndo kwanza wanasikia"

"Nataka niwaambie watu wa Arusha tunakazi ya kufanya ,kazi ya kutetea haki sio kazi rahisi ,kila wakikaa wanakuambia mbunge gani anagombana na kila mtu, kwenye wizi wa namna hii unataka maelewano mimi ningekuwa njaakali hawajamaa si wangeshanipa changu nikatulia"

Ends....






Post a Comment

0 Comments