DIWANI ARUSHA AMVUNJA MGUU MPIGA KURA WAKE KWA KIPIGO


Na Joseph Ngilisho ARUSHA

Diwani wa kata ya Amburen wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,Faraja Meliaki(CCM) anashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha Usa river kwa kosa la kumpiga na kumvunja mguu mwananchi wake,Erasto Mollel ambaye amelazwa katika hospitali  ya Rufaa ya Mt Meru mkoani hapa.

Diwani Faraja Meliaki aliyemvunja mguu mpiga kura wake ,picha hii alipiga akiwa kwenye kituo chake cha kulelea watoto yatima

Diwani huyo ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Faraja Orphanage ,anadaiwa kutenda tukio hilo la kinyama desemba 11 ,mwaka huu baada ya mwananchi  huyo kukataa kumuuzia shamba .


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo ila jitihada za kumtafuta ili kuthibitisha madai hayo zinaendelea.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi, Richard Ruyango alithibitisha tukio hilo na kudai kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumfikisha mahakamani diwani huyo .


Akiongea kwa uchungu Erasto Mollel ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa Mt Meru alidai kuwa siku ya tukio majira ya saa moja na nusu usiku ,diwani huyo alimpigia simu na kumtaka wakutane kwenye kijiwe cha kahawa eneo la kwa Fudu na alipofika walianza kurushiana maneno na baadaye diwani huyo alimrukia na kumvuja mguu na kukimbia.

"Baada ya kunivunja mguu diwani huyo na mwenzake walikimbilia kituo cha polisi Tengeru na kwenda kudai kuwa Mollel alimvamia na kumpiga madai ambayo sio kweli"alisema

Aidha Mollel amelitaka jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama hapa nchini ,kuchukua hatua juu ya diwani huyo kwani amekuwa akitishia amani kwa baadhi ya wananchi kwa kutumia fedha zake kujinasua na maovu ambayo amekuwa akiyatenda kwa wananchi na kwamba hilo sio tukio la kwanza kulitenda.


Mmoja ya wananchi wa kata hiyo,Jeremia kivuyo 
alidai kuwa diwani huyo amekuwa na tabia ya kunyanyasa wananchi huku akitumia vibaya fedha za wahisani wanaofika kutoa msaada katika kituo chake cha watoto yatima, kujinasua na matukio yake ya ovyo pindi anapofikishwa kituo cha polisi.

Ends...











Post a Comment

0 Comments