DC RUYANGO AHIMIZA MATUMIZI YA KINGA KWA VIJANA KWENYE MAHUSIANO


Na Joseph Ngilisho,ARUMERU 

MKUU wa wilaya ya Arumeru,mkoani Arusha, mhandisi Richard Ruyango, amewataka vijana wilayani humo sanjari na wale  wanaosoma  kwenye vyuo , kuhakikisha wanajitambua na  kujilinda na maambukizi ya ukimwi kwa kutumia kinga wanapokuwa kwenye mahusiano.

Mhandisi Ruyango ameyasema hayo katika chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru wilayani humo,wakati alipohudhulia maadhimisho ya siku ya udhibiti wa ukimwi duniani  ,ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Lindi.


Alisema maadhimisho hayo ambayo kiwilaya yalifanyika katika chuo hicho ,walilenga kutoa elimu zaidi kwa kuwakumbusha vijana kuwa Ukimwi bado upo na unaua hivyo nijukumu lao kama rasilimali ya taifa kujilinda na kuacha ngono uzembe.

"Vijana kama rasilimali ya taifa tunasisitiza kuhakikisha wanajilinda kwani ukimwi bado upo na unauwa hivyo katika chuo hiki chenye vijana takribani 4000  tunaweza tukawa tunapoteza vijana watano hadi sita kila mwaka bila sababu za msingi"alisema .

Alisema katika kipindi cha miaka 37 tangu janga la ukimwi limeingia nchini hakuna chanjo wala dawa iliyokwisha patikana ,ila dawa zilizopo nizakufubaza pekee,hivyo elimu tunayoendelea kuitoa ikawasaidie kuwakumbusha na lengo la serikali ni kuhakikisha watu wake wanabaki salama.


Alisema kuwa wilaya ya Arumeru ina kiwango cha asilimia 1.5 cha maambukizo ya ukimwi ,hivyo alisisitiza kuendelea kutolewa kwa elimu ya ukimwi kwa vijana hususani waliopo vyuoni .

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya alisema lengo la kufanyia maadhimisho hayo katika chuo hicho ni kuwafikishia elimu hiyo  vijana walio wengi ambao ndio waathirika wakubwa wa janga la ukimwi.


Aidha, Makwinya  amewaelekeza wakuu wa Idara za Afya na Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Meru kuhakikisha Elimu juu ya UKIMWI ni endelevu kwa vijana hao.

Awali mkuu wa taasisi ya maendeleo ya jamii ,dkt Bakari George alisema kuwa chuo hicho kimekuwa na utaratibu  wa kuwakutanisha wanachuo na wadau  ili kuwapatia mafunzo ya elimu ya afya ikiwemo maambukizi ya ukimwi ili kuwaimarisha  kisaikolojia.


Alisema hadi sasa wanachuo hao wamepata mafunzo mara sita na katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani wanafunzi hao waliadhimisha kwa kuchangia damu na kupima afya zao.



Ends...












Post a Comment

0 Comments