CHUO CHA UFUNDI ARUSHA , KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA YA MITAALA


Na Joseph Ngilisho,ARUSHA

CHUO cha Ufundi (ATC) Arusha, kimetakiwa kufanya mageuzi makubwa ya mitaala  ili  kiendane na mahitaji ya soko kwa wahitimu ,ukizingatia kwamba dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa elimu sayansi na teknolojia Prof.Maulilo Kipanyula wakati alipohudhulia mahafali ya 14 ya chuo cha Ufundi Arusha, ambapo jumla ya wahitimu 962 wa ufundi stadi ngazi ya ,Astashahada, Stashahada na Shahada walitunukiwa vyeti.


Alisema wizara ya elimu, sayansi na teknolojia  inatambua mchango mkubwa unaotolewa na chuo hicho katika kuendeleza sekta ya ujenzi na teknolojia nchini kupitia ushiriki katika miradi mbalimbali ya serikali na kuzalisha wataalamu waliobobea wa ufundi stadi  .

Alisema wizara ipo kwenye mchakato wa kufanya magezi makubwa ya elimu ,kisera na mitaala,hivyo alisema chuo hicho cha ufundi Arusha lazima kiendane na jitihada za wizara kufanya mageuzi ili yaendane na mahitaji ya soko.


"Mageuzi mtakayoenda kuyafanya mkumbuke kwamba dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda muangalie mahitaji ya soko yanahutaji wahitimu wa aina gani"

"Rais wetu amekuwa akisisitiza kuwa tutoe wahitimu wenye uwezo wa kujitegemea ,wahitimua ambao wakitoka wanaweza kufanya shughuli halali"


Prof Kipanyula alikipongeza chuo hicho kwa kukamilisha miradi mikubwa mitatu ya miundo mbinu ambayo ni  bweni la wasichana lenye uwezo wa kilaza wasichana 428,hospitali ya tiba na kujifunzia ,madarasa na maabara.

Awali mkuu wa chuo cha ATC dkt Mussa Chacha alisema kuwa chuo hicho kimeanza mradi wa ujenzi wa tawi la chuo hicho Kampasi ya Kikuletwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, unaofanyika kupitia mradi wa kujenga ujuzi kwa maendeleo na uingiliano  wa kikanda katika Afrika Mashariki(EASTRIP).


Alisema mradi huo unaofadhiliwa na benki ya dunia  utakuwa kituo cha Umahiri katika sekta ya nishati Jadidifu na tayari chuo kimesaini mikataba miwili na  kampuni ya ujenzi na ujenzi huo  umeanza.

Naye mwenyekiti wa bodi ya utawala ,Diana Mlambugi alisema bodi imekuwa ikifanya kazi kubwa kukabiliana na changamoto ya bajeti ya chuo kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoathiri utekelezzi wa majukumu ya chuo.

Alimshukuru rais Samia Suluhu kwa kuendelea kukipatia fedha chuo ili kuboresha miundo mbinu yake kipitia fedha za maendeleo zilizowezesha kulipa moshahara ,mafunzo viwandani ,chakula cha wanafunzi na  maendeleo ya chuo.

Ends..


Post a Comment

0 Comments