ASKARI POLISI ALIYETOROKA NA KIDHIBITI CHA MENO YA TEMBO ARUSHA,AKAMATWA.

 

Zawadi Ngailo, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha 

Na Joseph Ngilisho,Arusha


MMOJA ya Askari anayetuhumiwa kuhusika katika tukio la kuomba rushwa ya shilingi milioni 100, Kostebo Zakhayo kwa Mfanyabiashara Maarufu wa Mji wa Usa River Jijini Arusha,Profesa Justine Maeda na kufanikiwa kutoroka na ushahidi wa meno ya tembo amekamatwa na anashikiliwa katika kituo cha polisi Usa river ,wilayani Arumeru mkoani hapa. 

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha,Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Arusha,Justine Masejo alipoulizwa juu ya taarifa za kushikiliwa kwa Kostebo Zakhayo alisema kuwa jambo hilo lipo Takukuru ila anafuatilia kuona taarifa hizo zina ukweli kiasi gani.
Justine Masejo, Kamanda wa Polisi Arusha



"Mara ya mwisho suala hili lilikuwa ninashughulikiwa na Takukuru wenyewe hivyo sikujua kinachoendelea ila nitafuatilia kujua ukweli wa tukio hilo"alisema 

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo alithibitisha kukamatwa kwa askari polisi huyo ambaye alikutwa akiwa amejifisha kwa mwanamke mmoja eneo la Kimandolu jijini Arusha. 

"Kostebo Zahkayo alikamatwa jijini Arusha na uchunguzi zaidi  unaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani"

Akiongea kwa njia ya simu mwathiriwa wa tukio hilo, Profesa  Maeda alisema kuwa amesikia kukatwa kwa mtuhumiwa huyo akidai ni miongoni mwa askari waliogawana fedha zake ambaye alitoroka pia na kidhibiti cha meno ya tembo na mgawo wa sh,milioni 31 kati ya milioni 100 walizochukua.
Profesa Justine Maeda 



"Nimesikia askari huyo amekamatwa mimi ninachotaka ni fedha zangu tu wanirudishie mpaka sasa sijapata chochote"alisema prof Maeda.


Habari kutoka vyanzo vya ndani ya jeshi la polisi  Usa River, zilisema kuwa mtuhumiwa Kostebo Zakhayo alikamatwa Kijenge Juu kata ya Kimandolu Jijini Arusha nyumbani kwa mke wake alikoamua kurudi na kujificha baada ya kutokomea mafichoni kusikojulikana.

Kostebo Zahkayo na askari wenzake saba wakiwemo watano wa kituo cha polisi USA na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha na raia watatu wa mji wa Usariver walikamatwa na polisi Taarifa ambazo gazeti hili inazo zinasema kuwa tukio hilo lilitokea mapema march mwaka jana na askari waliokamatwa {majina tunahifadhi kwa sasa} ni pamoja Wakaguzi wasaidizi wawili {Inspekta},Askari Koplo mmoja na Askari Kostebo[PC} Wanne wawili ni wa kituo Kikuu cha polisi Arusha ambao walitoroka lindo na kwenda kufanya uhalifu huo wakiwa na silaha.

Ilidaiwa kuwa, mmoja ya raia watatu waliokamatwa (jina tunalihifadhi) aliwahi kuwa mfanyakazi katika shamba la profesa katika Mji wa Usariver na alifukuzwa kazi muda mrefu ndiye aliyeshawishi Polisi wadai rushwa kwa bosi wake wa zamani kwa madai kwamba ana mali nyingi na ni mwoga sana wa polisi.

Ilidaiwa kuwa, mtuhumiwa huyo aliwaeleza Polisi watafute meno ya tembo wayaweke kwenye moja ya mizinga ya nyuki shambani kwa mafanyabiashara huyo ili wamtuhumu kuwa anafanya biashara haramu na kwa kuwa ni muoga atakubali kutoa rushwa ya kiasi chochote cha pesa.


Ilidaiwa kuwa Polisi wa Usariver kwa kushirikiana na raia hao walitekeleza mpango huo na siku ya upekuzi Polisi wawili wenye silaha kutoka Arusha mjini walikwenda kwenye eneo la tukio ili kumuaminisha mfanyabiashara huyo kuwa upekuzi ni halali na na viongozi wa polisi Usa na Kituo Kikuu Arusha wanajua kitu ambacho sio kweli.

Taarifa zinadai kuwa shamba la mfanyabishara huyo lina mizinga mingi ya nyuki lakini katika upekuzi huo Polisi walikwenda moja kwa moja katika mzinga walikoficha meno ya tembo na kumuonesha mfanyabiashara huyo kuwa anafanya biashara haramu hivyo anastahili kushitakiwa kwa uhujumu uchumi.


Inadaiwa kuwa wakati wa upekuzi hakukuwa na kiongozi yeyote wa serikali wa Mtaa wala Balozi na hata ndugu wa karibu wa mtuhumiwa.


Vyanzo vya habari hizi vya Usariver na Arusha Mjini vinadai kuwa, mfanyabishara huyo aliwauliza Polisi wanahitaji kiasi gani ili kumaliza kesi hiyo wakasema walihitaji shilingi milioni 100.


Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo aliwapa shilingi milioni 74 alizokwenda kuchukua katika benki ya NMB na CRDB zilizoko katika Mji wa Usariver na kiasi kingine cha fedha cha shilingi milioni 26 aliomba kwa ndugu zake na kukamilisha kiasi cha shilingi milioni 100 walizoomba askari hao.

"Baada ya kunikamatisha meno ya tembo kwa kujiwekea kwenye mizinga yangu ya nyuki ,walitaka niwapatia sh,milioni 100 ili wasiende kunifungulia kesi ya uhujumu uchumi ,ndipo nilipoamua kuwapatia fedha hizo"alisema.

Aidha aliongeza kuwa askari hao baada ya kuona nimeenda kulalamika kituo cha polisi cha Usariver waliamua kunirudishia kiasi cha sh,milioni 26 huku wakisema kuwa fedha zingine wamepeleka kwa wakubwa zao sh,milioni 50.
 

 Ends...

Post a Comment

0 Comments