WIZARA YASUKA MKAKATI KABAMBE KUKUSANYA KODI YA PANGO LA ARDHI NCHINI

 


Na Joseph Ngilisho ,ARUSHA 


KATIBU Mkuu  wizara ya Ardhi  nyumba na maendeleo ya Makazi  Dkt Allan Kijazi amevitaka vituo vya makusanyo ya Kodi na masulufu ya serikali,kutozifumbia macho  taasisi za Serikali ambazo zinadaiwa kwa kuwa suala la ulipaji wa Kodi ni suala la kisheria na sio hiari. 
 

Dkt Kijazi aliyasema hayo mapema Leo jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mkakati wa makusanyo ya Kodi ya  pango la Ardhi  Kwa kushirikiana na benki ya CRDB.


Alisema kuwa ni muhimu  kwa  wamiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipa Kodi hizo Kwa wakati ili kuruhusu utekelezaji na mikakati mbalimbali ya kiserikali iweze kufikiwa 

Aliongeza kuwa kwa Sasa vituo vya makusanyo ya Kodi vinatakiwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote yule ambaye anaachwa hasa kwenye ukusanywaji wa Kodi na ikitokea hawajalipa ni muhimu hatua Kali na za kisheria ziweze kuchukuliwa.

 
"Kodi ni suala la kisheria na sio hiari taasisi  yeyote ambayo haijalipa kodi chukueni hatua kwa kuwa kutolipa Kodi ya pango ni sawa na ukiukwaji wa Sheria"aliongeza

Kwa upande wake kamishna wa ardhi nchini, Mathew Nhongwe alisema kuwa kama wizara mwaka huu wa fedha wamejipanga katika mwaka wa fedha 2022/23 kukusanya kiasi cha sh, billion 250  tofauti na mwaka jana walikusanya sh,bilioni 130.

Kamishna alisema wana mikakati mbalimbali ya kuendelea kukusanya Kodi ya pango la Ardhi Kwa kila mwananchi,taasisi za umma pamoja na binafsi

Aliongeza kuwa wamejipanga  kurahisisha zoezi la ulipaji tayari wa Kodi ya pango la Ardhi Kwa kushirikiana na taasisi na fedha.

"Leo tupo na CRDB tunataka kama mtu anataka kulipia Kodi yake iwe ni rahisi kwake asitembee umbali mrefu apate huduma karibu'

Hata hivyo taasisi za kifedha ikiwemo crdb Benk imeahidi kushirikiana bega Kwa bega na serikali kukusanya mapato yatokanayo sekta ya ardhi.

Ends...

Post a Comment

0 Comments