WAHITIMU CHUO CHA HOTELI NA UTALII VETA WATAKIWA KUKABILI FURSA YA AJIRA EAC

 

Naibu mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha idara ya Mipango,fedha na Utawala,dkt.Mogani Jilenga


Na Joseph Ngilisho Arusha 

WAHITIMU wa mafunzo ya hoteli na utalii katika chuo cha ufundi stadi (Veta) Arusha ,wametakiwa kuchangamkia fursa za ajira katika soko la jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kufuatia kufunguliwa kwa mipaka baina ya nchi wanachama.

Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na naibu mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha idara ya Mipango,fedha na Utawala,dkt.Mogani Jilenga wakati alipohudhulia mahafali ya 10 ya wahitimu wa chuo hicho ,ngazi ya Stashahada na Astashahada.


Alisema kuwa soko la ajira katika sekta ya hoteli na utalii hapa nchini mara nyingi linatekwa na raia wa nchi  jirani na kukosesha fursa kwa wazawa ,hivyo ni wakati mwafaka kwa wahitimu hao kutumia mtangamano wa soko la ajira la nchi wanachama wa EAC .

"Bila shaka mtakubaliana nami kuwa wakati huu ambapo jumuiya ya Afrika Mashariki imeimarika kuna changamoto ya kupanua wigo wa ajira baada ya kufunguliwa kwa mipaka baina ya nchi wanachama, hivyo wahitimu wote wanafsa ya kupata ajira katika nchi za EAC"


Dkt Jitenga aliwakumbusha wahitimu waliobaki kutumia fursa hiyo kwa kuongeza ushindani ,umahiri na ubunifu ili pindi wanapohitimu wawe na nafsi nzuri ya kujiajiri ama kuajiriwa.

Awali Kaimu Mkuu wa Chuo cha Veta ,Moshi ,Douglas Mlula aliyemwakilisha mkurugenzi wa Veta Kanda ya Kaskazini ,Monica Mbele,alisema kuwa chuo kina mpango wa kuongeza kudahili kutoka 400 wa sasa na kufikia wanachuo 500 ifikapo 2023 kwa kozi zote.


Aliongeza kuwa chuo kimekuwa na ushirikianao na vyuo na Taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo chuo cha utaluub,Kenya (KUC)Novartis Scotia Community College cha Canada ,Asilia,Grumeti,Tamisemi, Kamitei na Regrow.

Awali mkuu wa chuo hicho,Christopher Ayo alisema kuwa chuo kilianza mwaka 2011 kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na mafupi ikiwemo Upishi,mauzo ya vyakula ma vinywaji ,usafi wa Nyumba na Udobi na Uongozaji wa utalii.
Mkuu wa chuo cha ufundi stadi VETA,Christopher Ayo 


Mafunzo mengine ni usimamizi na uongozaji shughuli za utalii ,mapokezi na huduma za maradhi,Sanaa ya mapishi ,upambaji na uandaaji wa keki.

Hata hivyo alisema kuwa chuo kina changamoto  ya uhaba wa mabweli kwa ajili ya wanafunzi kulala.

Mkuu huyo wa chuo alitoa raia kwa jamii inayowazunguka kujenga hostel kwa ajili ya kuwapangishia wanafunzi wanaokuja kusoma katika chuo hicho .

Hata hivyo aliwataka wahitimu kuwa na moyo wa kujiajiri zaidi kuliko kuajiriwa kwa kuwa ujuzi watakuwa wamepata baada ya kufuzu mafunzo hayo.

Ends





 


Post a Comment

0 Comments