WAFANYAKAZI WAZINDUA SHIRIKISHO KUKABILI CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI AFRIKA

 

Na Joseph Ngilisho Arusha 


VYAMA vya wafanyakazi wa serikali za mtaa katika nchi za afrika ,zimezindua shirikisho la vyama vya wafanyakazi Afrika , AMALGUN lenye  lengo la kuimarisha umoja huo na kutatua changamoto za wafanyakazi kwenye nchi zao .

Akiongea mara baada ya kuzinduliwa kwa shirikisho hilo jijini Arusha,mwenyekiti Mpya wa Amalgun ambaye pia ni mwenyekiti chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania(TALGWU),Tumaini Nyamuhokya aliziomba nchi wanachama kuhakikisha zinajenga  mahusiano mazuri na vyama vya wafanyakazi  ili kuepusha migomo na maandamano yasiyo na tija.


Nyamuhokya ambaye pia ni Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania Tucta,alisema nchi zenye demokrasia afrika zina haki ya kuruhusu maandamano ya wafanyakazi  pale wanapokuwa wakidai maslahi yao.

Alisema mkutano huo ambao umeshirikisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutoka nchi saba wanachama afrika,pia kilifanya uchaguzi wa uongozi wa shirikisho hilo na  kukubaliana kuwa Arusha ,nchini Tanzania iwe makao makuu ya umoja huo.

"Maadhimio yetu katika kikao hiki ni kupitisha katiba tulioiunda nchini Ghana ,ikiwa ni pamoja na kufanya mkoa wa Arusha nchini Tanzania kuwa makao makuu wa shirikisho "

Mwenyekiti huyo aliziomba nchini wanachama kuwa na mahusiano mazuri na vyama vya wafanyakazi jambo litakalosaidia kuondoa migomo ya mara kwa mara  isiyo na tija. 

Naye katibu mkuu wa Amalgun,Roba Duba kutoka Kenya  alisema kwa zaidi ya miaka 10 vyama hivyo vilikuwa vikishirikiana kutafuta suluhu juu ya changamoto za wafanyakazi wa serikali za mitaa katika nchi zao.

Alisema hatua ya kuunda umoja huo  ni kutimiza malengo ya muda mrefu walioyatamani kwa muda mrefu na kilichopo mbele yao kwa sasa ni  kutatua migogoro iliyopo baina ya vyama vya wafanyakazi na nchi zisizo na demokrasia kupitia  nchini  zilizofanikiwa.


"Mambo ambayo yanatukabili afrika ni mengi tunachofanya kwa sasa ni kuungana ili kujaribu kutafuta uzoefu kwa nchi zilizofanikiwa "
 
Naye katibu Mkuu TALGWU, Rashird Mtima alisema lengo la muungano huo ni kutengeneza mtandao wa vyama vya wafanyakazi afrika waliopo kwenye sekta za serikali za mtaa ili kuhakiosha wanafanyakazi katika mazingira salama.


"Tupo hapa kubadilishana uzoefu ili kujua wenzetu wa nchi wanachama wanafanyaje katika kusimamia maslahi ya wafanyakazi bila kuwepo na migomo na hivyo tutakuwa na nafasi ya kuchota uzoefu na kuuhamishia nchini nyingine"

Ends..










Post a Comment

0 Comments