UKIHITIMU CHUO CHA HELF TO SELF HELP AJIRA NJE NJE


Na Joseph Ngilisho Arusha 


WAHITIMU wa mafunzo ya Upishi, Ususi,Umeme na ushonaji katika chuo cha Helf to Self help cha jijini Arusha, wametakiwa kutumia ujuzi walioupata kwenda kujiajiri na kuzalisha ajira kwa vijana .

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Baraza la Ngo's Tanzania,Lilian Badi kwenye Mahafali  ya 23 katika chuo cha Helf to Self help, ambapo wanachuo 67 walihitimu masomo yao.


Alisema kuwa changamoto kubwa inayowakumbwa wahitimu wa vyuo ni namna ya kupata fursa ya mikopo katika halmashauri kutokana na masharti magumu yanayosababisha vijana kushindwa  kujiajiri .

Aliiomba serikali kupitia rais Samia Suluhu kuwasaidia wadau waliowekeza kutoa elimu ya ujuzi kwa vijana wapunguziwe masharti ya mikopo waweze kuwaendeleza vijana na hivyo kupunguza wimbi la ajira  kwa vijana nchini.
 

Mwenyekiti  huyo wa baraza alitoa rai kwa wadau wa maendeleo hapa nchini kuzingatia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana ikiwemo kuwapatia vitendea kazi ili pale watakapo hitimu waweze kujiajiri.

Badi pamoja na kukipongeza chuo hicho kwa kutoa wahitimu bora ,aliahidi kuwapatia ajira wahitimu 10 kwa kuwaunganisha na taaisis mbalimbali waliohitimu sekta hizo.

Awali Mkurugenzi wa chuo cha Helf to Self help,Amani Golugwa alisema  chuo hicho tangu kuanzishwa kwake miaka 23 iliyopita kimechangia kwa kiwango kikubwa suala la Ajira nchini kutokana na umahili wa wahitimu.




Alisema kuwa chuo chake kimekuwa kiungo cha kuwaunganisha wajitimu na taasisi na wadau mbalimbali ili wapatiwe mikopo au vifaa fedha kwa ajili ya kujiajiri.


"Vijana wetu wengi waliohitimu katika chuo chetu wanakuwa wapo kwenye mpango wa ajira au kujiajiri na baadhi yao ndio watengenezaji mahili wa keki hapa nchini"alisema Golugwa.

Soko la ajira limekuwa likiwapokea vizuri walitimu hao na kutoa rai kwa wahitmu kuhakikisha wanaenda kuyaishi yale mema waliojifunza.

Ends...














Post a Comment

0 Comments