Dc Said Mtanda katikati akiongea na wamiliki wa bar na madj baada ya kuwachomoa lokapu |
Na Joseph Ngilisho Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Saidi Mtanda amewanusuru wamiliki wa kumbi za starehe pamoja na madj zaidi ya 50 waliokuwa wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi Jijini hapa, wasifikishwe mahakamani kutokana na kutenda makosa ya kuendesha biashara kinyume cha sheria ikiwemo kubughudhi watu kwa kufungulia mziki kwa sauti kubwa na kutokuwa na leseni.
Kwa mujibu wa Mtanda,watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia operesheni iliyofanywa usiku wa manane na halmashauri ya jiji la Arusha kupitia bodi ya video, baada ya kubaini kwamba wafanyabiashara wengi wa vileo wanaendesha shughuli zao kinyume cha sheria na hivyo kuikosesha mapato halmashauri hiyo.
Mmoja ya wamiliki wa bar jijini Arusha Fredrick Maimu ..akijaribu kujitetea baada ya kubanwa mbavu na DC. |
Mtanda alizitaja baadhi ya bar kinara wa matukio ya kupiga mziki kwa sauti kubwa kuwa ni pamoja na Picnic,Africana ,Arusha Live,Kipon'g,Bills,Darajani ,The Hub na kuagiza wamiliki wa bar hizo badala ya kupelekwa mahakamani watozwe faini na walipe kwa control namba.
Akiongea na wafanyabiashara hao pamoja na Madj ofisini kwake baada ya kufanikiwa kuwachomoa lokapu, walikosota kwa siku nne mfururizo na baadaye kuandaliwa mashtaka ya kupelekwa mahakamani jana.
Mtanda alisema alimwamuru Mkuu wa polisi wa wilaya ya Arusha,(OCD) Edith Swebe kuwaleta mbele yake mahabusu hao wakiwa na mashtaka Yao kila mmoja mkononi.
"Baada ya kupata taarifa kuwa Kuna madj na wamiliki wa bar wanashikiliwa kwa muda lokapu nilimwagiza OCD kabla ya kuwapeleka mahakamani awalete ofisini kwangu wakiwa na mashtaka Yao"
Hata hivyo alisema mara baada ya kukaa nao na kuwahoji kwa kina alijiridhisha kuwa wafanyabiashara hao wanaendesha biashara zao kinyume Cha sheria ikiwemo kutokuwa na leseni .
Alisema watu hao waliomba msamaha na ndipo mkuu huyo wa wilaya alipoamuru wasipelekwe mahakamani ila watozwe faini kwa mujibu wa sheria .
Naye kaimu mkurugenzi wa Jiji la Arusha,James Lobikoki alisema kuwa zoezi Hilo ni endelevu na limekuja baada ya kubaini kwamba wafanyabiashara wengi wanaendesha kumbi za starehe bila kufuata taratibu na hivyo kuikosesha mapato halmashauri hiyo.
"Sheria inakataza kupiga mziki ama kelele kwa sauti kubwa inayobughudhi wengine na nikosa kwa mujibu wa sheri na faini yake ni sh, milioni 5"alisema mwanasheria wa jijj la Arusha wakati akisoma vifungu vya sheria katika kikao hicho cha DC
Alisema katika operesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata Madj na wamiliki wa kumbi hizo zaidi ya 50 na hiyo ni baada ya kuwaonya mara kadhaa bila mafanikio.
"Zoezi letu tumeliendesha kwa mujibu wa sheria na tulikuwa tukipita kila bar kuanzia majira ya saa Saba usiku hadi saa Tisa na tulikamata madj na vyombo vyao vya mziki baada ya kukuta wamepitiliza muda uliopangwa kupiga mziki kwa sauti ambao ni mwisho saa SITA usiku "
Alisema wananchi wengi wanaoishi kando na kumbi za starehe wamekuwa wakilalamika kutopata usingizi kutokana na kelele za mziki jambo ambalo tumeona wanahaki kisheria na ndio maana tumeendesha zoezi Hili .
Ends...
.
0 Comments