TAZAMA UTAIPENDA HII! TRA ARUSHA ILIVYOADHIMISHA WIKI YA MLIPA KODI

 

Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Eva Raphael  alikabidhi msaada wa vyakula na sabuni kwa msimamizi mkuu mahabusu ya watoto jijini Arusha, James Kamugisha

Na Joseph Ngilisho,ARUSHA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Arusha imeadhimisha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi kwa aina yake pale ilipoamua kuwatembelea baadhi ya wafanyabiashara na kuwashukuru kwa kulipa kodi bila shuruti kwa maendeleo ya Taifa lao.

Aidha mamlaka hiyo imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na sabuni kwa mahabusu ya watoto jijini hapa,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi.

Akiongea na waandishi wa habari ,meneja wa TRA Mkoa wa Arusha ,Eva Raphael alisema kuwa mamlaka hiyo imeona umuhimu wa kuwatembelea  wafanyabiashara na kuwashukuru kwa kutambua umuhimu wa kulipa kodi bila kulazimishwa.
Eva Raphael, Meneja TRA mkoa wa  Arusha


Alisema kuwatembelea wafanyabiashara ni kujenga mahusiano bora baina ya mamlaka hiyo na wafanyabiashara ambao hapo awali waliiona TRA kama adui wa wafanyabiashara.

"Sisi kama mkoa tuliamua kutumia wiki hii kuwatembelea watoto wa walipa kodi  waliopo mahabusu na kuwaletea mahitaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mchango wetu wa huruma,kwani moyo usiokuwa na shukurani haupendezi"
Mfanyabiashara jijini Arusha Shose Mtei (kulia) akikumbatiana na meneja wa TRA ARUSHA Eva Raphael 


Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi,Richard Kayombo 
aliwashukuru wafanyabiashara mkoani hapa kwa kutambua umuhimu wa kulipa kodi kwani asilimia 60 ya mapato yanayokusanywa na TRA hurejea kwa wananchi kwa ajili ya huduma za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu.

Kayombo aliwaomba wafanyabiashara kuhakikisha wanaendelea na moyo huo wa kuona umuhimu wa kulipa kodi bila kusukumwa ili serikali iweze kutekeleza vema majukumu yake ya kuwaletea maendeleo.


Baadhi ya wafanyabiashara waliotembelewa,Lidya Kamando aiishukuru TRA kwa kuwatembea na kuwapatia elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwani kwa sasa wanaona kulipa kodi ni haki yao ya msingi  na sio kama awali walilazimika hata kufunga maduka kuwakimbia TRA.

Aliwaomba wafanyabiashara wenzake kutoiona TRA kama adui bali waone umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.

"Tunawaomba TRA muendelee kutoa elimu kwa wafanyabiashara wengi zaidi ili elimu nilioipata mimi aipate mtu mwingine  na aweze kulipa kodi bila kushurutishwa"alisema.

Mamlaka hiyo inatarajia kutoa tuzo kwa wafanyabiashra waliofanya vizuri katika sekta ya ulipaji kodi mzuri.

Ends..



Post a Comment

0 Comments