Na Joseph Ngilisho Arusha
Jiji la Arusha limekabidhi hundi ya mkopo yenye thamani ya sh, milioni 404.5 kwa vikundi 52 vya ujasiriamali kutoka kata 25 za jiji la Arusha.
Akiongea wakati wa kukabidhi hundi hiyo jana, kaimu mkurugenzi wa jijj la Arusha Hargeney Chitukulo,alisema mkopo huo ni awamu ya pili kwa vikundi vya ujasiriamali katika kutekeleza sheria ya kuviwezesha vikundi wa wanawake ,vijana na walemavu.
Alisema kati ya vikundi hivyo ,28 ni vya akina mama waliopata sh, milion 198.6 na vikundi 14 vya vijana waliopata sh, milioni 143.
Alisema wengine walionufaika na mkopo huo usio na riba ni vikundi 10 vya walemavu ,waliopata sh, milioni 62.9.
Chitukulo alisema kuwa mkopo awamu ya kwanza halimashauri hiyo ilitoa sh,873.6 kwa vikundi 118 ,vikiwemo 108 vya wanawake waliopatiwa sh, milioni 754.6.vikundi 10 vya vijana walipatiwa sh, milioni 118.9.
Alisema halmashauri ya jiji la Arusha imekuwa ikichangia maendeleo ya vikundi vya ujasiriamali kama sheria inavyowataka kupitia vikundi vya ufugaji ,biashara ndogondogo na vyombo vya usafiri .
"Tumekuwa tukiwapatia mafunzo kabla ya kupatiwa mkopo na leo watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali wa miradi yenye tija ,uongozi na usimamizi wa miradi ,utunzaji wa kumbukumbu za fedha , urejeshaji wa mkopo ,uandaaji wa taarifa ,afya ,Lishe na Bima "
Alisisitiza kuwa hali ya urejeshaji wa mikopo bado ni changamoto kubwa katika jiji la Arusha jambo inayosababisha fedha nyingi kubaki kwa wakopaji na kuwanyima haki hiyo vikundi vingine vyenye uhitaji.
Awali mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda aliwataka wakopaji kupitia vikundi vyao kuwa waadilifu na kutejesha mikopo hiyi kwa wakati.
Mtanda alimpongeza kaimu mkurugenzi wa jiji hilo Chitukuro kwa kufanikisha kutekeleza na kutoa fedha hizo akisema hayo ni matunda ya serikali chini ya Rais Samia Suluhu yenye lengo la kuwakwamu kiuchuni wananchi wake.
"Hakikisheni mikopo mliopewa mnarejesha kwa wakati ili vikundi vingine viweze kukopa msiende kutunia vibaya mkopo mliopewa"
Naye mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo, alisema kuwa kuna tabia kwa halmashauri ya jiji la Arusha kuchelewesha kuweka fedha kwenye akaundi ya vikundi mara baada ya kukabidhi hundi ya mfano.
Gambo alitaka fedha hizo zitolewe kwa wakati iili kuwapa fursa wakopaji wengine waliojiwekea malengo kufanya biashara zao na kuanza kurejesha.
Pia alisema kumekuwapo na baadhi ya wataalamu wa mikopo ambao wamekuwa wakidai rushwa kwa baadhi ya vikundi ili kupitisha maombi yao ya mkopo jambo ambalo lilikemewa na mkuu wa wilaya na kumtaka kaimu mkurugenzi kuhakikisha mikopo inatoka ndani ya wiki moja kama alivyoahidi.
Ends..
0 Comments