SAIMON IRANGHE MWENYEKITI MPYA UVCCM ARUSHA,AWAGARAGAZA VIBAYA WENZAKE


Na Joseph Ngilisho Arusha 


MTOTO wa Meya wa jiji la Arusha,Saimon Maximilian Iranghe ameibuka kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha (UVCCM).


Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo wa Vijana Mkoa wa Arusha Thomas Apson ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro alimtangaza kuwa mshindi, baada ya kupata kura  345 kati ya  kura  zilizopigwa. 555


Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo,Apson alisema uchaguzi huo uliofanyika kwanuhuru na haki katika ukumbi wa Simba Hall (AICC) jijini Arusha. 


Apson aliwashukuru wajumbe kwa kufanya uchaguzi wa uhuru na haki na kumtaka Mwenyekiti mpya  na Mwenyekiti alipita  kumaliza tofauti zao na kujenga chama imara.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka alisema  uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na kuwataka wajumbe kuendelea na chaguzi nyingine ndani ya Jumuiya zetu ngazi ya Mkoa.


" Pia niendelee kuwasihi wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha kuwa watulivu ili tuweze kumalizia chaguzi zetu salama ila msisahau kwenda kutangaza yale yote mazuri yanayofanyika na yanafanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndiye Rais wetu wa Awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan".


Kwa upande wake Mwenyekiti huyo mpya, Saimon Maximilian Iranghe aliwataka vijana wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba uchaguzi umeisha na wote sasa ni kitu kimoja.


“Makundi sasa yaishe, tunachotakiwa vijana wenzangu kwa sasa tufanye kazi kwa bidii na kujenga chama chetu,” alisema Saimon.


Aliwashukuru wapiga kura kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wapya pamoja na wale waliomaliza muda wao.


ends....


Post a Comment

0 Comments