RAIS SAMIA ATUNUKU KAMISHENI MAOFISA 724 TMA


BY NGILISHO NEWS ,Monduli 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Novemba 26, 2022 amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 724 wakiwemo wanawake 89 kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA)Monduli, Arusha.


Waliotunukiwa kamisheni hizo ni maofisa wanafunzi kundi la 03/19 shahada ya sayansi ya kijeshi na kundi la 69/21 refu pamoja na mahafali ya tatu ya shahada ya sayansi ya kijeshi kundi la 03/19 pamoja na wengine 20 waliohitimu nje ya nchi.

Tukio hilo limefanyika leo Novemba 26, 2022 katika chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) kilichopo Monduli Arusha.


“Mimi Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa madaraka niliyopewa Katika ibara ya 148 kifungu kidogo cha pili kifungu kidogo  cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu cha 29 kifungu kidogo cha 5 cha sheria ya ulinzi wa Taifa.


“Ninawapa kamisheni kuwa maofisa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania katika cheo cha Ruteni Usu kuanzia leo Novemba 26, 2022,” amesema Rais Samia.


Pamoja na hayo, awali Rais Samia Suluhu Hassan amekabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi darasani na katika nafasi mbalimbali kimasomo.


Akizungumza awali, Mkuu wa chuo cha mafunzo Monduli, Brigedia Jenerali Jackson Moseba amesema wanafunzi waliohitimu wanajumuisha kozi mbili, ambapo jumla ya maofisa wanafunzi 724 wametunukiwa huku wengine wakishindwa kumaliza masomo kutokana na sababu mbalimbali.


Amezitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na utoro, kukosa nidhamu, maombi binafsi, utimamu wa mwili na matatizo mengine.

Post a Comment

0 Comments