Na Joseph Ngilisho Arusha.
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Mawakili wa Afrika ya Mashariki kuwa wazalendo na kuzimamia haki wanapotekeleza majukumu yao katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki kwa kuzingatia misingi ya demokrasia .
Samia aliyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 22 wachama cha Mawakili wa Afrika ya Mashariki (EALS), jijini Arusha.
Rais Samia alisema lengo la kuwa na jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuwaunganisha wananchi, kuleta amani, utulivu na kusaidia kukuza uchumi wa mataifa yao.
Pia, Rais Samia aliwataka mawakili hao kuhakikisha wanasimamia haki katika utekelezaji wa kazi zao ili kuhakikisha amani na utulivu vinadumu katika Afrika ya Mashariki.
Katika mkutano huo, Rais Samia alitoa rai kwa mawakili hao kusimama pamoja kama Waafrika wa Afrika ya Mashariki hasa katika kukabiliana na changamoto za utandawazi, teknolojia na masuala ya ikolojia kwa kufanya kazi kwa pamoja lakini kwa kuzingatia historia, tamaduni na desturi za kila nchi.
Rais Samia alikubali maombi ya chama hicho kupatiwa ardhi ya ujenzi wa makao makuu lakini pia kurahisisha ufanyaji wa kazi kwa ushirikiano baina ya mawakili wa nchi wanachama.
Awali, Rais wa EALS, Bernard Oundo aliomba kuboresha mazingira ya mawakili kufanyakazi ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, kupata ardhi ya ujenzi wa makao makuu ya EALS.
Ends...
0 Comments