RPC Arusha, Justine Masejo |
Na Joseph Ngilisho Arusha
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha katika kuhakikisha linakomesha matukio ya ajali kuelekea mwisho wa mwaka katika Mkoa limewafungia leseni za udereva madereva watano wanaotoka na usugu wa makosa ya barabarani ikiwemo ulevi.
Akitoa taarifa hiyo leo kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo alisema kuwa madereva hao wamefungiwa leseni zao kwa muda wa miezi mitatu hadi sita kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo ulevi.
Kamanda alija makosa mengine kuwa ni mwendokasi, kusababisha ajali, wenye makosa yanayojirudiarudia pamoja na wale ambao wanayapita magari mengine (overtaking) sehemu ambazo zimekatazwa kisheria.
Kamanda Masejo alisema pamoja na adhabu hiyo ,Jeshi hilo limefanikiwa kutoa elimu katika nyumba za ibada, stendi za mabasi, mashuleni, vijiwe vya bodaboda pamoja na masoko ambapo jamii hiyo imepata uelewa wa kutosha kuhusiana na sheria mbalimbali za usalama barabarani.
Aidha ACP Masejo alitoa onyo kali kwa madereva wanaoendele kuvunja sheria za usalama barabarani kuwa Jeshi hilo halito muonea muhali dereva yeyote kwa makosa ya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani.
Pia amewaomba wananchi kutoa taarifa za uhalifu na walifu ili kuuufanya Mkoa huo kuwa shwari.
Ends..
0 Comments