PICHA :MAZIKO YA DEREVA BODABODA HUYU NI KASHESHE HAIJAWAHI KUTOKEA ,SOMA UJIONEE


Na Joseph Ngilisho Arusha 

WAENDESHA  Bodaboda zaidi ya 400 wilaya ya Arumeru wamezua taharuki katika mazishi ya mwenzao,Shadrack Loserian  baada ya kuvuruga ibada ya mazishi kanisani kwa kuunyakua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika kwenye kaburi bila ndugu kuhusishwa.

Vituko hivyo vya aina yake vilianza majira ya asubuhi wakati ndugu na jamaa wakichukua mwili wa marehemu katika hospitali  ya mkoa Mt Meru na kisha kuelekea katika kijiji cha Olgilai,wilayani humo,ambako taratibu za maziko zilikuwa zimeandaliwa .

Kwa mujibu wa shuhuda wa vioja hivyo vya waendesha pikipiki hao,vilianza kwa kulazimisha kutembea na jeneza la marehemu kwa kulazimisha kulibeba kutoka Moshwale hadi katika kijiji hicho umbali wa zaidi ya kilometa 30.

"Pia wakiwa kaburini walikuwa wakipiga kelele na kutupia jeneza kama la kibaka katika kuburi hilo, hii sio haki kabisa "alisema Jonathan Mollel 

Hatua hiyo ililazimu ndugu wa marehemu kuita polisi ili kuwatawanya vijana hao waliokuwa wakipiga kelele na kuendesha pikipiki kwa fujo huku wakipiga honi jambo lililozua taharuki na Sintofahamu,hata hivyo polisi baada ya kufika walishindwa kuchukua hatua yoyote na kuacha vijana hao kuendelea na vurugu zao,ingawa hazikuwa na athali ya uvunjifu wa amani.

"Hao waendesha pikipiki walikuwa wengi sana na walileta vurugu kubwa kwa kupiga kelele wakilazimisha kuubeba mwili  wa mwenzao jambo lililopigwa na ndugu walidai wamelipia gari kwa ajili ya kubeba jeneza la marehemu"alisema Samweli Kivuyo ambaye ni ndugu wa marehemu.

Aliongeza mara baada ya kufika kanisani jeneza liliingizwa kanisani na wakati mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Oigilai akiendelea na ibada ya maombi ghafla kundi la vijana hao walivamia kanisa na kuondoka na jeneza hilo.

Alisema vijana hao baada ya kufika kaburini waliingiza jeneza ndani ya kaburi na kuanza kufukia udongo kwa kutumia mikono huku wakizuia ndugu wa marehemu wala mchungaji kufika katika kaburi hilo.

Baba wa marehemu Edward Loserian alieleza kusikitishwa na kitendo cha vijana hao akidai kwamba kitendo hicho kimemnyima haki ya msingi ya kuuzika mwili wa mwanaye kwa kufuata taratibu zote za maziko.

Tangu nizaliwe sijawahi kuona kitendo cha aina hii kilichofanywa na hawa vijana naiomba serikali idhibiti matukio ya aina hii kwani yanaonesha kukomaa katika jiji la Arusha kwa vijana kuteka maziko kwa sababu kuwa eti alikuwa mtu wao wa karibu.

Hata hivyo Loserian alisema kuwa hakubahatika hata kuaga mwili wa mwanaye ambaye alifariki akiwa nyumbani baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Ends...





Post a Comment

0 Comments